Pata taarifa kuu

Vita katika Ukanda wa Gaza: Wakaazi wanahofia tishio la kushambuliwa Rafah

Idara ya kUjasusi ya Israel inasema Hamas ilikataa mpango wa kusitisha mapigano uliopendekezwa Jumapili Aprili 14. Jeshi la Israel, kwa upande wake, linabaini kwamba mateka wanashikiliwa mjini Rafah na linakumbusha vitengo viwili "kwa ajili ya shughuli za uendeshaji kwenye eneo la Gaza", bila kutoa maelezo mengine, na hivyo kuacha hatari ya operesheni huko Rafah.

Wapalestina, waliokimbia makwao kutokana na mashambulizi ya Israel, wanaishi katika makambi ya hema kwenye mpaka na Misri huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 10, 2024.
Wapalestina, waliokimbia makwao kutokana na mashambulizi ya Israel, wanaishi katika makambi ya hema kwenye mpaka na Misri huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 10, 2024. © Mohammed Salem / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu katika Ramallah, Alice Froussard

Huko Gaza, bado kunasikika milipuko ya mabomu na mizinga. Vita havijasimama na Wapalestina wanahofia kwamba vitashika kasi kutokana na matamshi ya hivi punde ya Israel. Kwa vyovyote vile, hivi ndivyo Fares, mtu aliyefukuzwa kutoka Gaza, anaamini. "Shambulio dhidi ya Iran sio muhimu sana kwetu. Tunataka tu kurudi majumbani mwetu. Tumemelazimika kuyahama makaazi yetu. Tunasubiri kuona kitakachotokea katika saa chache zijazo, kuona kama Israel itaijibu Iran au ikiwa inajaribu tu kugeuza tahadhari kutoka kwa shambulio lijalo la Rafah,” anaeleza mkaazi huyo wa Gaza.

"Vita nyingine ya kisaikolojia"

Israel, kwa kuwaitisha askari wa akiba, kwa mara nyingine tena inazusha tishio la mashambulizi dhidi ya Rafah, ambapo zaidi ya watu milioni 1.5 waliokimbia makazi yao wamekusanyika. “Vita nyingine ya kisaikolojia,” anasema Aya, mwenye umri wa miaka 25. “Hakuna tena sehemu salama hapa. Nadhani jeshi lina mpango huu akilini ya kutuondoa katika miji yote. Hakuna kitakachotufaa. Kilichobaki ni kutuombea tu, ni hayo tu,” anashuhudia mkazi huyo ambaye bado kijana.

Baadhi ya watu wa Gaza hasa wanaogopa wakati, wakibaini kwamba Marekani haitaizuia Israel katika maeneo mawili kunaripoitwa vita: huko Gaza na vita dhidi ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.