Pata taarifa kuu

Gaza: Mossad ya Israel yasema Hamas imekataa mpango wa kusitisha mapigano

Mossad, idara ya ujasusi ya Israel, imesema leo Jumapili kwamba Hamas ya Palestina imekataa mpango wa hivi karibuni wa kusitisha mapigano uliowekwa mezani wiki moja mapema mjini Cairo na wapatanishi.

Yahya Sinwar (wa pili kulia), kiongozi mpya wa vuguvugu la Kiislamu la Hamas katika Ukanda wa Gaza na kiongozi mkuu wa kisiasa Ismail Haniyeh (kushoto) ameketi karibu na mtoto wa Mazen Faqha, kiongozi wa Hamas ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana huko Gaza.
Yahya Sinwar (wa pili kulia), kiongozi mpya wa vuguvugu la Kiislamu la Hamas katika Ukanda wa Gaza na kiongozi mkuu wa kisiasa Ismail Haniyeh (kushoto) ameketi karibu na mtoto wa Mazen Faqha, kiongozi wa Hamas ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana huko Gaza. ©MAHMUD HAMS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kukataliwa kwa pendekezo lililowasilishwa na nchi tatu zinazopatanisha katika mazungumzo hayo - Marekani, Misri na Qatar - kunaonyesha kuwa kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, Yahya "Sinwarr hataki makubaliano kwa ajili ya misaada ya kibinadamu, wala kurejea kwa mateka," inabaini Mossad (kitengo cha masuala ya kigeni cha idara ya ujasusi ya Israeli), katika taarifa kwa vyombo vya habari katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, saa chache baada ya shambulio la Iran dhidi ya Israel.

Taarifa zaidi zinakujia...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.