Pata taarifa kuu

Usitishwaji vita Gaza: Rasimu ya azimio la Marekani yapingwa na kura mbili za turufu

Urusi na China "zimepiga kura ya turufu" mnamo Ijumaa Machi 22 azimio la Marekani katika Umoja wa Mataifa likisisitiza "haja" ya usitishaji mapigano "haraka" huko Gaza, na balozi wa Urusi akilaani rasimu "ya kinafiki" ambayo haitowi wito wa moja kwa moja wa kusitishwa kwa mapigano. 

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. ©REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Rasimu ya azimio la Marekani, ambayo inasisitiza juu ya "haja ya usitishaji vita wa haraka na wa kudumu" kuhusiana na kuachiliwa kwa mateka, imepata kura 11 za ndio, kura tatu zikipinga (Urusi, China na Algeria) na moja ya Guyana, ikijizuia kutoa msimamo wowote.

Kushindwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha rasimu hii ya azimio, kwa mara nyingine tena kumezimwa na mzozo wa kidiplomasia kati ya mataifa makubwa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekataa, Ijumaa hii, Machi 22, azimio lililotolewa na Marekani kuhusu "kusitisha mapigano mara moja" katika Ukanda wa Gaza, ambapo zaidi ya watu 31,000 wameuawa tangu vita kuanza Oktoba 7, kulingana na Wizara. wa Afya katika eneo hilo, linalodhibitiwa na Hamas.

Kimsingi, maandishi hayo yalisisitiza “haja ya usitishaji vita wa mara moja na wa kudumu ili kulinda raia kutoka pande zote, kuwezesha utoaji wa msaada muhimu wa kibinadamu […], na kwa kuzingatia hili, inaunga mkono bila shaka juhudi za kidiplomasia za kimataifa kufikia usitishaji huo wa mapigano kuhusiana na kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa. Nchi kumi na moja, zikiwemo Marekani, Ufaransa na Uingereza zilipiga kura ya ndiyo, mataifa matatu - China, Urusi na Algeria, nchi pekee ya Kiarabu kwenye Baraza hilo - yamepinga, Guyana ilijizuia.

Mshirika mkuu wa Israel, Washington hadi wakati huo ilikuwa inapinga matumizi ya neno "kusitisha mapigano. Marekani imezuia mara tatu maazimio ya Umoja wa Mataifa kwa athari hii kwa kutumia haki yao ya kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini uungwaji mkono kutoka Marekani umepungua kwa muda wa wiki kadhaa, kutokana na ghasia za mashambulizi ya Israel dhidi ya eneo lililoharibiwa na mabomu na kutishiwa na njaa, lakini pia kutokana na shinikizo la mrengo wa kushoto wa Marekani, ambalo linasukuma utawala wa Joe Biden kubadilika nafasi yake miezi michache kabla ya uchaguzi wa rais. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye aliwasili Israel Ijumaa hii kama sehemu ya ziara nyingine ya kidiplomasia, alielezea azimio la Washington siku ya Jumatano jioni kama "ishara kali".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.