Pata taarifa kuu

Gaza: Saudi Arabia yatangaza msaada wa dola milioni 40 kwa UNRWA

Saudi Arabia imetangaza siku ya Jumatano kutoa mchango wa dola milioni 40 (karibu euro milioni 37) kwa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), ambapo Israel inalishtmu kwa wafanyakazi wake kuhusika katika shambulizi la hivi karibuni kwenye ardhi yake.

Le siège endommagé de l'Office de secours et de travaux des Nations Unies pour les réfugiés de Palestine (Unrwa) dans la ville de Gaza, le 15 février 2024.
Makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) yaliyoharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel katika Jiji la Gaza, Februari 15, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Fedha hizo zitasaidia "juhudi za misaada ya kibinadamu za UNRWA katika Ukanda wa Gaza", unaokumbwa na vita kati ya Israel na Hamas, kwa kutoa "chakula kwa zaidi ya watu 250,000 na mahema kwa familia 20,000," kulingana na taarifa kutoka kwa  Kituo cha Msaada wa Kibinadamu na Usaidizi cha Mfalme Salman (KSrelief).

"Ni muhimu kukabiliana na mahitaji ya wakazi wa Gaza" wanaotishiwa na njaa kulingana na Umoja wa Mataifa, ameongeza mkuu wa KSrelief, Abdallah al-Rabeeah. Israel inaishutumu UNRWA kwa kuajiri "zaidi ya magaidi 450" huko Gaza na inadai kuwa wafanyakazi wake 12 walihusika moja kwa moja katika shambulio la Oktoba 7 ambalo halijawahi kushuhudiwa lililotekelezwa na Hamas katika ardhi ya Israel.

Nchi kadhaa zimesitisha misaada yao

Shirika hilo linaloajiri takriban watu 30,000 katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu pamoja na Jordan, Syria na Lebanon, limeachana na wafanyakazi wanaotuhumiwa.

Lakini karibu nchi kumi na tano, haswa Marekani, zilisitisha ufadhili wao mwishoni mwa mwezi wa Januari baada ya shutuma za Israeli. Tangu wakati huo, nyingi miongoni mwa nchi hizi zimeanza tena kutoa michango yao.

UNRWA ni uti wa mgongo wa misaada ya kibinadamu huko Gaza, ambapo karibu watu 32,000, wengi wao wakiwa raia, wameuawa katika operesheni za kijeshi za Israeli za kulipiza kisasi, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas.

Kulingana na taarifa ya Saudia kwa vyombo vya habari, Philippe Lazzarini, mkurugenzi wa UNRWA, amebaini kwamba mchango wa Saudi Arabia "unaonyesha mshikamano ambao nchi hii ya kifalme imekuwa ikionyesha kwa Wapalestina".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.