Pata taarifa kuu

Iran: Mazishi ya wahanga wa shambulio la Kerman yafanyika

Maelfu ya watu wamekusanyika Kerman kushiriki katika mazishi ya wahanga wa shambulio la mabomu mawili ambalo liligharimu maisha ya watu zaidi ya 80 na karibu mia tatu kujeruhiwa siku ya Jumatano Januari 3. Umati wenye hasira ukidai kulipiza kisasi.

Ukipiga kelele "kisasi, kisasi," "kwa Israeli" na "kwa Marekani," umati mkubwa ulimtaka kiongozi wa Walinzi wa Mapinduzi kulipiza kisasi cha vifo vya makumi ya watu, wakiwemo wanawake 44 na watoto, waliouawa wakati wa shambulio la mabomu mawili Jumatano Januari 3 huko Kerman. Picha imetolewa na ikulu ya rais wa Iran.
Ukipiga kelele "kisasi, kisasi," "kwa Israeli" na "kwa Marekani," umati mkubwa ulimtaka kiongozi wa Walinzi wa Mapinduzi kulipiza kisasi cha vifo vya makumi ya watu, wakiwemo wanawake 44 na watoto, waliouawa wakati wa shambulio la mabomu mawili Jumatano Januari 3 huko Kerman. Picha imetolewa na ikulu ya rais wa Iran. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi

Ukipiga kelele "kisasi, kisasi," "kwa Israeli" na "kwa Marekani," umati mkubwa ulimtaka kiongozi wa Walinzi wa Mapinduzi kulipiza kisasi cha vifo vya makumi ya watu, wakiwemo wanawake 44 na watoto, waliouawa wakati wa shambulio la mabomu mawili Jumatano Januari 3 huko Kerman. Mkuu wa kikosi maalumu cha Iran amethibitisha kwamba vifo vya watu hao vimelipizwa kisasi mapema kwa msaada uliotolewa kwa makundi mbalimbali yanayopigana hivi sasa na Israel huko Gaza lakini pia kupitia vitendo vya Hezbollah, Houthi nchini Yemen au hata makundi ya Kishia huko Iraq na Syria.

"Ahadi ya Mungu"

Akielekeza hotuba yake kwa wapiganaji wa kundi la Islamic State lililodai kuhusika na mashambulizi hayo mawili, Jenerali Hossein Salami amesema: "Nyinyi ni maafisa wa utawala wa Kizayuni na Marekani tu." Kwa upande wake, Rais wa Iran Raïssi kwa mara nyingine tena alinyooshea kidole cha lawama taifa la Kiyahudi, akithibitisha kwamba mwisho wa Israeli uko karibu: "Leo, wanaua wanawake na watoto huko Gaza. Lakini tunajua kwamba hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu na kwamba mwisho wa mafuriko ya Al-Aqsa utakuwa mwisho wa utawala wa Kizayuni. Insha'Allah".

Kulipiza kisasi ni "kiwango cha chini" ambacho adui lazima atarajie, ameongeza rais wa Irani. Licha ya matamko haya, bado haijulikani jinsi mamlaka ya Irani itafanya, lakini shambulio hili la mabomu mawili hakika litachochea mzozo katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.