Pata taarifa kuu

Shambulio dhidi ya hospitalini Gaza: Uturuki kutangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Uturuki itatangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya shambulio katika hospitali moja huko Gaza ambao ulisababisha vifo vya mamia na ambapo Israel na Palestina wanatuhumiana, afisa mkuu wa Uturuki ameliambia shirika la habari la AFP, akithibitisha habari kutoka kwa vyombo vya habari kadhaa vya ndani. 

Kwa mujibu wa naibu kiongozi wa chama tawala cha AKP bungeni, Özlem Zengin, aliyenukuliwa na televisheni ya serikali ya Uturuki TRT na kituo cha kibinafsi chaa NTV, tangazo hilo litatolewa rasmi kwa agizo la rais
Kwa mujibu wa naibu kiongozi wa chama tawala cha AKP bungeni, Özlem Zengin, aliyenukuliwa na televisheni ya serikali ya Uturuki TRT na kituo cha kibinafsi chaa NTV, tangazo hilo litatolewa rasmi kwa agizo la rais via REUTERS - MURAT CETINMUHURDAR/PPO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa naibu kiongozi wa chama tawala cha AKP bungeni, Özlem Zengin, aliyenukuliwa na televisheni ya serikali ya Uturuki TRT na kituo cha kibinafsi chaa NTV, tangazo hilo litatolewa rasmi kwa agizo la rais.

Hayo yanajiri wakati Wizara ya Afya ya eneo la Palestina linalodhibitiwa na Hamas, likisema takriban watu 471 waliuawa katika shambulio la anga lililopiga jengo la hospitali ya Al Ahli Arab katika Ukanda wa Gaza.

Hili ndilo shambulio baya zaidi kutekelezwa huko Gaza baada ya vita kati ya Israeli na kundi la Hamas, zaidi ya wiki moja iliyopita.

Hali hiyo imesababisha kufutwa kwa mkutano nchini Jordan, ambako rais Biden alikuwa akutane na viongozi wa nchi za Kiarabu.

Tangu kuanza kwa vita hivyo, Oktoba 7 baada ya kundi la Hamas kushambulia Israeli,  Wapalestina zaidi ya 3,000 wameuwa kwenye ukanda wa Gaza huku Waisraeli zaidi ya  1,400 wakipoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.