Pata taarifa kuu

Rais Joe Biden amewasili nchini Israeli

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili nchini Israeli kwa ziara ya kuonyesha mshikamano na taifa hilo kufuatia shambulio la kundi la Hamas.

Ziara hiyo inalenga kuonyesha mshikamano kati ya mataifa hayo kufuatia shambulio la Hamas dhidi ya Israeli
Ziara hiyo inalenga kuonyesha mshikamano kati ya mataifa hayo kufuatia shambulio la Hamas dhidi ya Israeli AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo pia inakuja wakati huu shambulio kwenye hosipitali moja katika eneo la Gaza ambalo limesababisha vifo vya karibia watu mia tano likizua hofu ya kutokea kwa uhasama zaidi katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.

Rais Biden anazuru wakati huu Israeli na Hamas zikiendelea kutuhumiana kutokana na shambulio katika hosipitali mjini Gaza
Rais Biden anazuru wakati huu Israeli na Hamas zikiendelea kutuhumiana kutokana na shambulio katika hosipitali mjini Gaza AP - Evan Vucci

Biden amepokelewa na waziri mkuu Israeli Benjamin Netanyahu wawili hao wakionekana kukumbatiana katika uwanja wa ndege ishara ya mshikamano baina yao.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya kikao jijini Tel Aviv
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya kikao jijini Tel Aviv AP - Evan Vucci

Mamia ya walinda usalama waliojihami wameonekana katika hoteli seafront mjini Tel Aviv, eneo ambako Netanyahu na Biden wanatarajiwa kuwa na kikao.

Tel Aviv iko kilomita 65 sawa na maili 40 kutoka katika ukanda wa Gaza, makao ya wapiganaji wa Hamas ambao Israeli imekuwa ikiwakabili tangu shambulio la Oktoba 7.

Israeli imeapa kupambana na wapiganaji wa Hamas inayowaita kuwa magaidi
Israeli imeapa kupambana na wapiganaji wa Hamas inayowaita kuwa magaidi AP - Evan Vucci

Ziara hii inakuja wakati huu pia kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis akitoa wito wa hatua kuchukuliwa kupesha eneo  la Gaza kuinga katika mzozo wa kibinadamu.

Aidha Papa Francis ameonya kuhusu uwezekano wa kupanuka kwa mzozo wa Israeli na Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.