Pata taarifa kuu

Misri yapinga Wapalestina kuondoka Ukanda wa Gaza kwenda Sinai

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi ameonya siku ya Jumatano Oktoba 18 dhidi ya idadi kubwa ya Wapalestina kutoka Gaza kwenda Misri. Rais wa Misri anaona hatari ya "kama hiyo ya watu kuondoka Ukingo wa Magharibi kuelekea Jordan" na huenda ukawa "mwisho wa kile wanapigani kama taifa huru la Palestina".

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Cairo Oktoba 15, 2023.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi wakati wa mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Cairo Oktoba 15, 2023. AFP - JACQUELYN MARTIN
Matangazo ya kibiashara

Wakati akimpokea Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Cairo Jumatano hii, Oktoba 18, Abdel Fattah al-Sissi ametoa hotuba yake ya kina na kali tangu kuanza kwa vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas. Mzozo huo tayari umesababisha maelfu ya watu kuuawa kwa pande zote mbili na milioni moja wamelazimika kuyahama makazi yao katika eneo hilo dogo la Wapalestina linalo kabiliwa na mashambulizi ya Israel kwa siku 12. Wengi wao walikimbilia kusini, kwenye mpaka karibu na Misri.

Kulingana na rais wa Misri, kuwasukuma Wapalestina kuondoka katika ardhi yao ni "njia ya kukomesha kile wanachopigania kwa manufaa ya nchi jirani".

"Wazo la kuwalazimisha Wagaza kwenda Misri litasababisha Wapalestina kuondoka Ukingo wa Magharibi," eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel. "Na hii itafanya kuanzishwa kwa Taifa huru la Palestina kutowezekana," ameongeza. Ikiwa nitawauliza watu wa Misri waingie mitaani, kutakuwa na mamilioni ambao wataunga mkono msimamo wa Misri," ameonya, akitaja pia "maoni nyeti ya Waarabu" na "maoni ya Waislamu" kwa kutetea taifa huru la Palestina."

Muda mfupi baada ya tamko hili, maelfu ya Wamisri walimiminika mitaani katika miji mbalimbali ya nchi hiyo yenye watu wengi zaidi katika nchi za Kiarabu, kwa mshikamano na Ukanda wa Gaza, inayokumbwa na mashambulizi ya anga ya Israel kwa siku 12, kulingana na picha zilizorushwa na vyombo vya habari vya ndani na kwenye mitandao ya kijamii katika nchi hiyo ambapo kuandamana ni haramu.

Wakati ulimwengu ukitoa wito wa kufunguliwa kwa kivuko cha Rafah kati ya Misri na Gaza, Bw. Sissi amekariri kwamba nchi yake "haijafunga kivuko cha Rafah" na haijaingia katika ardhi ya Palestina kwa sababu "mashambulio ya anga ya Israel. Kwa siku kadhaa, mamia ya malori yamekwama katika jangwa la Sinai nchini Misri, kwa sababu ya kutoweza kupita kwa takriban watu milioni 2.4 wa Gaza, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) sasa likithibitisha kwamba "kila sekunde tunaposubiri msaada wa matibabu, tunapoteza watu.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.