Pata taarifa kuu

Mfalme wa Jordan aonya juu ya kulazimishwa kwa Wapalestina kuhamia nchi jirani

Abdullah II, Mfalme wa Jordan, ameonya juu ya kulazimishwa kwa Wapalestina kuhamia nchi jirani au kusini mwa Gaza.

Mfalme Abdullah II wa Jordani, katika Baraza la Wawakilishi huko Amman, Machi 23, 2021.
Mfalme Abdullah II wa Jordani, katika Baraza la Wawakilishi huko Amman, Machi 23, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unasema kiasi hiki kinafikia takriban watu milioni 1.1 - karibu nusu ya wakazi wa Ukanda wote wa Gaza.Eneo lililoathiriwa ni pamoja na Mji wa Gaza wenye wakazi wengi.

"Umoja wa Mataifa unaona kuwa haiwezekani kwa harakati kama hiyo kufanyika bila matokeo mabaya ya kibinadamu," Umoja wa Mataifa ulisema katika taarifa yake.

Jeshi la Israel limeuambia Umoja wa Mataifa kwamba kila mtu anayeishi kaskazini mwa Wadi Gaza anapaswa kuhamia kusini mwa Gaza katika muda wa saa 24 zijazo, anasema msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Israel imekuwa ikijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini, kukusanya wanajeshi, mizinga mikubwa na vifaru kwenye mpaka wa Gaza.

Imekuwa ikiafanya mashambulizi ya anga mjini Gaza tangu Jumamosi baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel kwa kushtukiza.

Umoja wa Mataifa unasema Gaza inakabiliwa na hali "mbaya" kutokana na chakula na maji kuisha haraka na wajawazito 50,000 hawawezi kupata huduma muhimu.

Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani linasema wafanyakazi 11 wa matibabu wameuawa huko Gaza tangu Jumamosi.

Zaidi ya watu 1,400 wameuawa huko Gaza tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi, huku watu 338,000 wakikimbia makazi yao.

Idadi ya Waisraeli waliouawa na Hamas wakati wa mashambulizi yake mwishoni mwa juma imeongezeka hadi 1,300, huku mateka wasiopungua 150 wakipelekwa Gaza.

Wakati huo huo, waziri wa habari wa Israel, Galit Distel Atbaryan, amejiuzulu - akisema ufadhili wa idara hiyo utatumika vyema kwingineko.

Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula Von Der Leyen atazuru Israel siku ya Ijumaa kuelezea mshikamano wake na wahanga wa mashambulizi ya Hamas.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pia anasafiri kuelekea Israel siku ya Ijumaa- siku moja baada ya ziara ya waziri wa mambo ya nje Antony Blinken.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.