Pata taarifa kuu

Takriban wanajeshi 258 wa Israel wameuawa tangu shambulio la Hamas

Takriban wanajeshi 258 wa Israel wameuawa tangu shambulio la umwagaji damu lililoanzishwa tarehe 7 Oktoba na kundi la wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina dhidi ya Israel, jeshi la Israel limesema Ijumaa, Oktoba 13.

Jeshi la Israel linaendelea na operesheni yake kuelekea katikati mwa Gaza.
Jeshi la Israel linaendelea na operesheni yake kuelekea katikati mwa Gaza. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

"Familia za wanajeshi 258 ambazo zimewapoteza wapendwa wao zimefahamishwa rasmi," msemaji wa jeshi Daniel Hagari amesema katika mkutano na wanahabari. Ripoti ya awali inaonyesha askari 169 waliuawa, shirika la habari la AFP linabaini.

Wakati huo huo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imetoa ombi la dharura ikizitaka nchi kutoa $294m (£241m) kwa ajili ya ufadhili wa dharura wa mahitaji ya haraka zaidi ya Wapalestina.

Fedha hizo zitatumika kuwasaidia baadhi ya watu milioni 1.2, shirika hilo lilisema.

Zaidi ya watu 84,000 katika mji wa Gaza walikosa makazi siku ya Alhamisi, shirika hilo lilisema, na kuongeza kuwa sasa kuna zaidi ya watu 423,000 wasio na makazi huko.

Haya yanajiri wakati Israel iliamuru raia wa Ukanda wa Gaza kuhamia kaskazini mwa eneo la Palestina lililoko Gaza ndani ya saa 24, kauli agizo lililopigwa vikali na Hamas. Umoja wa Mataifa unasema unahofia "matokeo mabaya ya kibinadamu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.