Pata taarifa kuu

Israel yaamuru 'raia wote wa Gaza' kuhama kusini ndani ya saa 24

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban watu milioni 1.1 wameamriwa kuhama kutoka kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini ndani ya saa 24, huku waziri mkuu wa Israel akiapa "kuiangamiza" Hamas.

Wakaazi wa Ukanda wa Gaza karibu na makazi yao baada ya uvamizi wa Israeli, Oktoba 12, 2023.
Wakaazi wa Ukanda wa Gaza karibu na makazi yao baada ya uvamizi wa Israeli, Oktoba 12, 2023. AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, jeshi la Israel lilitoa wito siku ya Ijumaa, Oktoba 13 ikiwataka "raia wote katika mji wa Gaza kuhama makazi yao kuelekea kusini kwa usalama wao na ulinzi wao na kuhamia eneo la kusini mwa Wadi Gaza", eneo linalopatikana kusini mwa jiji. "Kwa usalama wenu na wa familia zenu, kaeni mbali na Hamas ambayo inawatumia kama ngao za kibinadamu," inasema taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, ambayo pia inatoa wito kwa wananchi wa Gaza kutokaribia mpaka na Israel. "Mtaruhusiwa tu kurejea katika Jiji la Gaza wakati tangazo jingine la kuruhusu hili litatolewa," jeshi liliongeza.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, ambao hapo awali uliarifiwa juu ya agizo hili la "kuhama", agizo hili linahusu takriban watu milioni 1.1 kati ya wakaazi milioni 2.4 wa eneo hilo. "Agizo hilo linatumika kwa wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa na wale wote wanaopewa hifadhi katika vituo vya Umoja wa Mataifa - ikiwa ni pamoja na shule, vituo vya afya na kliniki," msemaji wa Antonio Guterres, Stéphane Dujarric, amesema.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) lilitangaza siku ya Ijumaa kuhamisha kituo chake cha operesheni na wafanyakazi wake hadi kusini mwa Ukanda wa Gaza. "UNRWA imehamisha kituo chake cha operesheni na wafanyakazi wa kimataifa kuelekea kusini, ili kuendelea na shughuli zake za kibinadamu na msaada kwa wafanyakazi wake na wakimbizi wa Kipalestina huko Gaza," shirika hilo limeandika kwenye ukurasa wake ya X (zamani ikiitwa Twitter).

Hamas "yafutilia mbali" agizo la raia kuhama

Saa chache kabla, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliahidi, baada ya mkutano mjini Tel Aviv na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kuangamiza Hamas. "Kama vile ISIS walivyokandamizwa, Hamas itaangamizwa," waziri mkuu alisema, akimaanisha kundi la Islamic State.

Kuni la wanamgambo wa Kiislamu kutoka Palestina, Hamas limefutilia mbali agizo hili linalowataka raia kuhamia kusini mwa Gaza. "Watu wetu wa Palestina wanakataa tishio la viongozi wa (Israel) na wito wao wa kuondoka makwao na kukimbilia kusini au Misri," ilisema taarifa hii. “Sisi tuko imara kwenye ardhi zetu, katika nyumba zetu na katika miji yetu. Hakuna mtu atakayehama,” iliongeza Hamas.

Hapo awali, mkuu wa huduma ya vyombo vya habari vya Hamas alisema tangazo la Israel ni "propaganda za uwongo" zilizokusudiwa "kuzua mkanganyiko" kati ya wakaazi wa Gaza na kuharibu "mshikamano wa ndani." Salama Marouf aliwataka Wagaza kutokubali kutii agizo la Israeli.

"Hali mbaya"

Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake, ulionya kwamba kuondolewa kwa kiwango kama hicho "haiwezekani bila kusababisha athari mbaya za kibinadamu". Katika mazingira haya, "Umoja wa Mataifa umesema ikiwa agizo hili limethibitishwa, kufutwa ili kuzuia kile ambacho tayari ni janga kuwa hali ya janga zaidi," alisisitiza.

"Jibu la Umoja wa Mataifa kwa onyo la hapo awali la Israel kwa wakazi wa Gaza ni la aibu," alijibu Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa Gilad Erdan katika ujumbe uliotumwa kwa shirika la habari la AFP na idara zake, akishutumu Umoja wa Mataifa kwa "kufumbia macho Hamas ambayo inatumia silaha na kutumia Ukanda wa Gaza kuficha silaha zake”. "Sasa, badala ya kusimama na Israel, ambayo raia wake waliuawa na magaidi wa Hamas, na ambayo inajaribu kuzima uharibifu kwa wale waliohusika, Umoja wa Mataifa unaitahadharisha Israel," alishutumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.