Pata taarifa kuu

Cairo yapendekeza misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza kupitia ardhi yake

Wito na mazungumzo ya kutuma misaada ya kibinadamu huko Gaza, inayozingirwa na Israel, kupitia Misri umeongezeka katika muda wa saa 48 zilizopita. Shehena ya kwanza ya msaada wa kibinadamu iliwasili Alhamisi kutoka Jordan.

Wakaazi wa Ukanda wa Gaza wanatoroka makazi yao baada ya uvamizi wa Israeli huko Rafah, Oktoba 2, 2023.
Wakaazi wa Ukanda wa Gaza wanatoroka makazi yao baada ya uvamizi wa Israeli huko Rafah, Oktoba 2, 2023. AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

Misri iliziita, Alhamisi, Oktoba 12, nchi zote na mashirika yanayotaka kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu wa Palestina ili kuusafirisha kupitia uwanja wa ndege wa al Arich, huko Sinai Kaskazini, anaripoti mwandishi wetu huko Cairo, Alexandre Buccianti. Al Arich iko takriban kilomita hamsini kutoka kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah, sehemu pekee ya kuvukia isiyodhibitiwa na Israel.

Wito huu kutoka Misri wa "upatikanaji wa haraka na salama" wa misaada ya kibinadamu kwa Gaza ulitolewa baada ya mazungumzo yaliyofanywa na rais wa Misri na mkuu wa diplomasia. Majadiliano yalifanyika hasa na Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa nia ya kuunda ukanda wa kibinadamu kutoka Misri hadi Gaza.

WHO inasisitiza wito wake wa ukanda wa kibinadamu

"Nina wasiwasi sana" juu ya hali hiyo, mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus, siku ya Alhamisi alisisitiza wito wa kuunda ukanda wa kibinadamu ili kupeleka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. "Tunahitaji ukanda, kutoa huduma za matibabu" na msaada wa chakula kwa Gaza, aongeza, akizindua upya wito wa WHO uliyozinduliwa siku ya Jumanne. Alikwenda Cairo siku ya Jumatatu kwa mkutano wa kikanda wa shirika hilo, na alizungumza na mkuu wa nchi wa Misri Abdel Fattah al-Sissi.

Kuanzia siku ya pili ya mashambulizi ya anga, Misri ilitangaza kuwasilisha msafara mkubwa wa kibinadamu. Hata hivyo, msafara huu ulipunguzwa hadi malori machache kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel ambayo yalisababisha kufungwa kwa mpaka wa Rafah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.