Pata taarifa kuu

Kenya yaonya dhidi ya mashambulizi ya Al Shabab 'kwa mshikamano na Hamas'

Polisi ya kupambana na ugaidi nchini Kenya imeonya Alhamisi kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya makundi yenye silaha, kama vile wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali wa Kisomali, Al Shabab, ambayo yatatekelezwa kwa "mshikamano na Hamas".

Kulingana na polisi ya Kenya ya kukabiliana na ugaidi, "makundi ya kigaidi kama Al Shabab yanaweza kufanya mashambulizi kwa mshikamano na Hamas ili kuonyesha kuwa bado wana nguvu."
Kulingana na polisi ya Kenya ya kukabiliana na ugaidi, "makundi ya kigaidi kama Al Shabab yanaweza kufanya mashambulizi kwa mshikamano na Hamas ili kuonyesha kuwa bado wana nguvu." © AFP - LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

Kenya, ambayo inaunga mkono taifa la Kiyahudi katika mashambulizi yake dhidi ya vuguvugu la Kiislamu la Palestina, imekuwa ikilengwa mara kwa mara na kundi la Al Shabab, kundi lenye mfungamano na Al-Qaeda, tangu uingiliaji wake wa kijeshi kusini mwa Somalia mwaka 2011, kisha ushiriki wake katika kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Amisom, ambayo kwa sasa ni Atmis) iliyoundwa mwaka 2012 ili kukabiliana na uasi huu.

"Makundi ya kigaidi kama Al Shabab yanaweza kufanya mashambulizi kwa mshikamano na Hamas ili kuonyesha kuwa bado yana nguvu zaidi," polisi ya Kenya ya kukabiliana na ugaidi imesema kwenye "X" (zamani ikiitwa Twitter). "Wakenya lazima wawe waangalifu na kuripoti vitendo vya kigaidi kwa polisi ili kuchukuliwa hatua," polisi imeongeza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ililaani katika taarifa yake siku ya Jumamosi, "kwa maneno makali zaidi, shambulio lisilo la wanamgambo wa Hamas dhidi ya watu wa Israeli", lililotekelezwa siku hiyo. "Kitendo hiki cha kikatili sio tu kimevuruga amani tete katika Mashariki ya Kati, lakini pia ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa kimataifa," imeandika.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Al Shabab ilitoa uungaji wake mkono kwa Hamas ambayo ilizindua Oktoba 7, katikati ya Shabbat, mapumziko ya kila wiki ya Wayahudi, shambulio ambalo hakijawahi kushuhudiwa nchini Israeli.

Mamia ya wapiganaji wa Hamas waliingia nchini humo kwa magari, kwa ndege na wengine kutumia njia ya baharini, kuua zaidi ya raia elfu moja, wakieneza hofu kwa kurusha roketi kutoka Ukanda wa Gaza. Takriban Waisraeli 150, wageni na watu wenye uraia pacha, walichukuliwa mateka na Hamas, kulingana na serikali ya Israel.

Israel ilijibu kwa kutangaza vita vya kuharibu uwezo wa Hamas, kwa kushambulia kwa makombora Ukanda wa Gaza na kupeleka makumi ya maelfu ya wanajeshi kuzunguka eneo la Palestina na kwenye mpaka wake wa kaskazini na Lebanon. Kwa upande wa Wapalestina, idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya mabomu ilikuwa 1,354 siku ya Alhamisi, kulingana na mamlaka ya Gaza.

Kenya, nchi jirani ya Somalia, iliadhimisha mwezi Septemba mwaka wa kumi wa shambulio baya lililotekelezwa na Al Shabab dhidi ya kituo cha biashara cha Westgate katika mji mkuu wa Nairobi, ambapo watu 67 waliuawa.

Mnamo 2015, Al Shabab walishambulia Chuo Kikuu cha Garissa mashariki mwa Kenya, na kuua watu 148, karibu wote wakiwa wanafunzi. Mnamo 1998, shambulio la bomu lililotekelezwa na Al-Qaeda dhidi ya ubalozi wa Marekani huko Nairobi liliua watu 213.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.