Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Syria: Wanajeshi wa Kikurdi na IS waendelea na vita vikali vya kudhibiti jela

Mapigano yamekuwa yakiendelea usiku wa Jumamosi Januari 22 kuamkia Jumapili Januari 23, kwa siku ya tatu mfululizo, kati ya kundi la Islamic State na vikosi vya Wakurdi kaskazini mashariki mwa Syria, kufuatia shambulio kubwa la wanajihadi dhidi ya jela, na kuua karibu watu 90. Lakini idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi, kwani hatima ya makumi ya walinzi na wafungwa bado haijulikani, kulingana na Shirika la Haki za Binadamu la Syria, OSDH.

Raia wa Syria wanakimbia makazi yao katika kitongoji cha Ghwayran katika mji wa kaskazini wa Hasakeh Januari 22, 2022, ikiwa ni siku ya tatu ya mapigano kati ya kundi la Islamic State (IS) na vikosi vya Wakurdi nchini Syria baada ya IS kushambulia gereza kulikokuwa kukizuiliwa wanajihadi katika eneo hilo.
Raia wa Syria wanakimbia makazi yao katika kitongoji cha Ghwayran katika mji wa kaskazini wa Hasakeh Januari 22, 2022, ikiwa ni siku ya tatu ya mapigano kati ya kundi la Islamic State (IS) na vikosi vya Wakurdi nchini Syria baada ya IS kushambulia gereza kulikokuwa kukizuiliwa wanajihadi katika eneo hilo. © AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Wakurdi vikisaidiwa na helikopta kutoka muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani walifanya mashambulizi Jumamosi jioni katika jaribio la kutwaa tena gereza la Ghwayran katika mji wa Hassakeh.

Kituo kikubwa zaidi duniani cha kunakozuiliwa wanajihadi, ambapo wapiganaji 3,500 wa kundi la Islamic State, wakiwemo viongozi wakuu, wamefungwa, kiko chini ya udhibiti wa kundi hilo la itikadi kali tangu siku ya Alhamisi, baada ya uhasama ndani ya jela hilo uliochochewa na uvamizi kutoka nje.

Wafungwa walikamata silaha za kijeshi, ikiwa ni pamoja na magari yaliyokuwa na bunduki nzito na silaha za kurusha roketi.

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria limeripoti kuwa eneo linalozunguka gereza hilo limechukuliwa, ingawa linaripoti mapigano ya hapa na pale katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande mwingine, jela hilo bado lilikuwa mikononi mwa kundi la Islamic State Jumamosi jioni.

Zaidi ya wanajihadi 130 waliotoroka jela walikamatwa. Lakini wengine kadhaa walifanikiwa kupenya, linasema shirika hilo lisilo la kiserikali yenye makao yake makuu nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.