Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Ufaransa: Mwanamume mmoja akamatwa na kushtakiwa kwa kulipatia jeshi la Syria vifaa

Mwanamume huyo,raia wa Ufaransa menye asili ya Syria, anashukiwa kuwa alitoa vifaa vinavyoweza kutumika kutengeneza silaha za kemikali, kinyume na vikwazo vya kimataifa dhidi ya Syria.

Mpiganaji wa Jeshi la Syria akisindikiza msafara wa Umoja wa Mataifa ukiwa umebeba timu ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kwenye moja ya maeneo ya shambulio linalodaiwa kuwa la silaha za kemikali kwenye viunga vya Damascus.
Mpiganaji wa Jeshi la Syria akisindikiza msafara wa Umoja wa Mataifa ukiwa umebeba timu ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kwenye moja ya maeneo ya shambulio linalodaiwa kuwa la silaha za kemikali kwenye viunga vya Damascus. REUTERS/Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

Mashtaka ni makubwa. Kulingana na chanzo cha mahakama kilichohojiwa na RFI, Mfaransa huyo mwenye uraia wa Syria aliyekamatwa tarehe 20 Desemba anashtakiwa kwa "njama ya kutenda uhalifu dhidi ya binadamu, kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita na pia utapeli wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ".

Mtu huyo ambaye utambulisho wake haujafichuliwa anashukiwa kulipatia jeshi la Syria vifaa vilivyokusudiwa kufuatilia na kukandamiza raia, kati ya mwaka 2011 na 2019 na kutoa vifaa ambavyo vinaweza kutumika kutengeneza silaha za kemikali, kinyume kabisa na vikwazo vya kimataifa dhidi ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.