Pata taarifa kuu
SYREIA-USALAMA

Syria: IS yachukua udhibiti wa gereza lenye wanajihadi 3,500 wakiwemo viongozi muhimu

Wanajeshi 18 wa vikosi vya usalama vya Kikurdi wameuawa pamoja na wanajihadi 39 wa kundi la Islamic State, IS, katika shambulio la kundi la Islamic State kwenye gereza moja katika mji wa Hassakeh kaskazini mashariki mwa Syria.

Picha ya zamani ya tarehe 26 Oktoba 2019: Watu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State (IS) walikusanywa katika chumba kimoja cha jela katika jiji la Hassakeh kaskazini mashariki mwa Syria.
Picha ya zamani ya tarehe 26 Oktoba 2019: Watu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State (IS) walikusanywa katika chumba kimoja cha jela katika jiji la Hassakeh kaskazini mashariki mwa Syria. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Asubuhi ya Ijumaa, Januari 21, mapigano yaliendelea ndani na nje ya jela, kwa mujibu wa Shirika la Haki za Kibinadamu nchini Syria la OSDH na vyanzo vilivyo karibu na Damascus.

Saa kadhaa baada ya shambulio dhidi ya gereza la Ghwayran katika mji wa Hassaké, pamoja na shambulio kutoka nje, vikosi vya Wakurdi bado vilikuwa havijadhibiti tena kituo hicho siku ya Ijumaa asubuhi.

Shirika la Haki za Binadamu la Syria limeripoti kuwa mamia ya wapiganaji wa kundi la Islamic State walidhibiti gereza hilo baada ya kukamata silaha na risasi za wanajeshi hao.

Mkakati makini kwa upande wa IS

Wanajihadi walichochea mapigano kati ya wafungwa baada ya kuendesha shambulio nje ya jela. Wapiganaji wa kundi la Islamic State walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari ndogo na lori la mafuta karibu na lango kuu la jela.

Wanajeshi wa serikali ya Syria na vikosi vya Syrian Democratic Forces, SDF, wakiungwa mkono na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, wanagawana udhibiti wa mji huu mkubwa kaskazini mashariki mwa Syria.

SDF wametuma idadi kubwa ya vikosi kujaribu kudhibiti hali hiyo, wakisaidiwa na helikopta za muungano ambazo zinafanya doria karibu na jela hilo, huku sheria ya kutotoka nje ikitangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.