Pata taarifa kuu
UJERUMANI-HAKI

Afisa wa zamani wa idara ya upelelezi Syria ahukumiwa kifungo cha maisha Ujerumani

Mahakama nchini Ujerumani, imemhukumu Anwar Raslan aliyekuwa Kanali katika jeshi la Syria, maisha jela baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa binadamu, katika Gereza moja karibu jiji la Damascus, miaka 10 iliyopita.

Anwar Raslan (katikati), katika chumba cha mahakama cha Koblenz, Ujerumani magharibi, Januari 13, 2022.
Anwar Raslan (katikati), katika chumba cha mahakama cha Koblenz, Ujerumani magharibi, Januari 13, 2022. AFP - THOMAS FREY
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Mahakama umepongezwa na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu duniani ukiongozwa na Human Rights Watch, kwa kile walichokieleza ni wa kihistoria kwa wananchi wa Syria ambao waliteseka mikononi mwa rais Bashar al-Assad.

Mahakama imempata Kanali Raslan kwa makosa ya mauaji,mateso, ubakaji udhalilishaji wa kimapenzi.

Viongozi wa mashtaka waliieleza Mahakama namna Raslan alipanga kuwateseka watu zaidi ya 4,000 katika gereza la Al-Khatib, kati ya Aprili 2011 hadi Septemba 2012, na kusababisha vifo vya watu 58.

Aidha, imeelezwa kuwa wafungwa  hao waliteswa kwa kwa umeme na kupigwa vikali.

Huu ndio uamuzi wa Kwanza wa historia kuhusu mzozo wa Syria, dhidi ya Kanali huyo wa zamani wa jeshi la Syria aliyekamatwa mwaka 2019 baada ya kukimbilia nchini Ujerumani mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.