Pata taarifa kuu
UN-SYRIA

Misaada yakwama siku nyingine kukiwa na hofu ya mapigano Aleppo

Msafara wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa vita jimboni Aleppo nchini Syria imekwama kwa siku nyingine wakati huu vikosi vya syria na wapiganaji waasi nje ya jiji la Damascus wakizua wasiwasi kuhusu kuongezwa kwa muda wa kusitsiha mapigano.

Hofu ya mapigano imetanda jimboni Aleppo baada ya kusua sua kwa makubaliano ya Marekani na Urusi
Hofu ya mapigano imetanda jimboni Aleppo baada ya kusua sua kwa makubaliano ya Marekani na Urusi REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Ghasia za ijumaa zilielezewa kama hatari zaidi tangu makubaliano yaliyoanza kutekelezwa jumatatu huku pande zote mbili waasi na serikali zikituhumiana kuvunja makubaliano yaliyofikiwa na Urusi na Marekani.

Ishara nyingine iliyoibua mvutano ni Washington kuiambia Moscow kuwa ushirikiano wa kijeshi nchini Syria hautawezekana hadi pale itakapoishinikiza serikali ya Syria kuruhusu kupelekwa kwa misaada katika maeneo yanayodhibitiwa.

Hayo yanajiri wakati Urusi ikiituhumu Marekani kwa kukataa kulishirikisha baraza la usalama la umoja wa mataifa hati za makubaliano ya kumaliza mapigano nchini Syria.

Mkutano wa dharura wa baraza umeitishwa kujadili makubaliano ambayo yaliahirishwa ghafla ijumaa kufuatia kupishana na Marekani na Urusi juu ya mkataba wa pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.