Pata taarifa kuu
SYRIA-VITA

Syria: Aleppo yagawanyika, huku mapigano yakibisha hodi

Katika mji wa Aleppo, raia wamekua na wasiwasi ya kuzuka mapigano kwa wakati wowote kati ya jeshi la Syria, muungano wa wanajihadi na waasi. Mapigano makali yametokea kusini magharibi mwa mji huo, yakilengwa na mashambulizi ya anga ya ndege za Urusi na Syria.

Kifaru cha waasi wa Syri katika eneo la Ramoussa, kusini magharibi mwa mji Aleppo Agosti 2.
Kifaru cha waasi wa Syri katika eneo la Ramoussa, kusini magharibi mwa mji Aleppo Agosti 2. REUTERS/Abdalrhman Ismail/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Urusi imetangaza kusitisha mapigano kwa muda wa saa tatu kati ya 4 asubuhi na 7 mchana saa za Syria, kila siku kuanzia Alhamisi hii, ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingiakatika mji huo. Umoja wa Mataifa unasema muda huo hautoshi, ukiomba usitishwaji wa mapigano kwa muda wa siku mbili mfululizo .

Pande zote mbili zimeendelea kujidhatiti kwa silaha za kivita pembezoni mwa mji wa Aleppo kwa maandalizi ya vita. Chanzo kilio karibu na kundi la Hezbollah mjini Beirut, kimeithibitishia RFI kwamba askari wa ziada wa vikosi maalum vya jeshi la Syria pamoja na wapiganaji wa Lebanon na Iran tayari wametumwa katika maeneo mbalimbali yanayouzunguka mji huo.

Waasi kwa upande wao, wamesema wanataka kuzidisha idadi mara mbili. Katika hali hii, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema Jumatano Agosti 10, kwamba wapiganaji 7000 wa makundi ya kijihadi wamekusanyika karibu na mji wa Aleppo.

Katika uwanja wa vita, hali ni tete. Jeshi la Syria na washirika wake wameendelea na mashambulizi yao, ili jaribio kufunga barabara iliyofunguliwa na waasi, ambayo inaelekea katika maeneo ya mashariki yanayozingirwa na majeshi ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.