Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-MOSUL

Iraq: raia watoa ushahidi kwa masaibu yanayowakumba Mosul

Ni mwaka mmoja sasa , tangu Mosul, mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq, uangake mikononi mwa wanajihadi. Tangu wakati huo, wakazi wa mji huo walikimbia kwa wingi na idadi ya wakaazi wa mji wa Mosul ikapungua kutoa milioni nne hadi milioni mbili.

La ville irakienne de Mossoul a été conquise par les jihadistes du groupe Etat islamique il y a un an.
La ville irakienne de Mossoul a été conquise par les jihadistes du groupe Etat islamique il y a un an. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Raia ambao wamebaki katika mji huo wamekua wakipata mateso, kwani Mosul imekua kama gereza. Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu (Islamic State) imetoa marufuku ya kuondoka katika mji huo na kulazimisha raia kuishi chini ya utawala wa ugaidi. Mkazi wa Mosul ambaye amefanikiwa kutoroka, ametoa ushahidi wa masaibu yote hayo yanayowakuta raia waliobaki katika mji huo.

Kwenye simu, mkazi huyo amesisitiza kutotaja jina lake. Raia huyo ambaye amefanikiwa kuondoka katika mji wa Mosul amesema anahofia usalama wa familia yake iliyobaki katika mji huo, ambapo zaidi ya watu wananyimwa mahitaji ya msingi. Katika mji wa Mosul, ambao unadhibitiwa na wanajihadi tangu mwaka mmoja uliyopita, raia huyo amesema watu wamekua wakifariki kutokana na njaa na ajira zimekosekana, huku shughuli zote zikikwama.

" Hali kwa kweli ni ngumu. Hali ya maisha pia ni ngumu. Familia hazina tena uwezo, wala pesa za kukidhi mahitaji yao ya msingi. Watu hawana kazi, hakuna ajira. Wanajihadi wa Daech pekee ndio wana uwezo ", amesema raia huyo.

" Kutokana na hali hiyo baadhi ya familia wamekua wakijaribu kuondoka Mosul lakini hawaruhusiwi. Wale ambao wamekua wakiruhusiwa kuondoka wamekua wakilazimishwa kutoa dhamana. Wanapaswa kutoa dhamana, hususan nyumba zao au hata mali zao ", ameongeza raia huyo.

Hali ngumu inayowakabili wakaazi wa Mosul, kwa mujibu wa raia huyo, imewekwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu kwa lengo maalum: " Kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, baadhi ya vijana hujiunga na wanajihadi ambao huwalipa mishahara midogo kwa malipo ya Dola 150- hadi 200 kwa mwezi ".

Wanajihadi ni “wakweli”, kwa mujibu wa mkazi mwengine wa Mosul

Katika jamii ya Wasuni, ambao wameendelea kutengwa na utawala wa Baghdad, wamekaribisha kuwasili kwa wanajihadi wa Islamic State, wakibaini kwamba ni ukombozi kwao.

“ Nakuapieni kuwa wanajhadi wanatenda haki kwa sasa. Nakuapieni, kwakweli. Sijawasifu sana, lakini ni wakweli. Wakati unapeleka mashataka mbele yao, hata kama ni mmoja wao wanamuadhibu ”, amesema Abou Mahmoud, mkazi wa Mosul.

Abou Mahmoud amesema wapiganaji wa Daech hawajihusishi na mauaji kama inavyodaiawa na wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.