Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-MAPIGANO-USALAMA

Iraq: “ kunahitajika wapiganaji wa kujitolea dhidi ya IS”

Serikali ya Iraq inatoa wito wa kujitokeza kwa wapiganaji wa kujitolea kulisaidia jeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State katika mji wa Ramadi.

Wapiganaji wa Islamic State wakiweka bendera za kundi hilo pembezoni mwa barabara za mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo la Al-Anbar, Jumatatu Mei 18 mwaka 2015.
Wapiganaji wa Islamic State wakiweka bendera za kundi hilo pembezoni mwa barabara za mji wa Ramadi, mji mkuu wa jimbo la Al-Anbar, Jumatatu Mei 18 mwaka 2015. AFP PHOTO / HO / AAMAQ NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Iraq imekiri kutokuwa na wanajeshi wa kutosha katika eneo hilo na hivyo imekuwa ni sababu ya kuelemewa na Islamic State.

Maelfu ya wakaazi wa Ramadi wamekimbia makwao baada ya Islamic State kuuchukua mji huo.

Marekani inasema inatekeleza mashambulizi ya angaa kuwadhoofosha wapiganaji hao na kufanikiwa kwa Islamic State mjini Kobane kunarudisha nyuma mafanikio ya Operesheni hiyo.

Rais Barrack Obama amemwambia mshauri wake wa maswala ya usalama Susan Rice kuja na mpango wa kuisiadia Iraq ikiwemo kuanza mara moja kuwapa silaha wanajeshi hao lakini pia kuwapa mafunzo zaiidi.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya wakaazi elfu 20 wa mji huo wameyakimbia makwao tangu Jumapili iliyopita baada ya kuingia kwa Islamic State.

Mbali na Iraq Islamic State wanadhibiti maeneo kadhaa nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.