Pata taarifa kuu
MAREKANI-UFARANSA-IS-SYRIA-IRAQ-USALAMA

Matokeo ya mkutano wa muungano dhidi ya IS

Muungano wa kimataifa unaoendesha vita dhidi ya Islamic State umekutana Jumanne wiki hii na kufanya tathimini kuhusu hatua yake ya kupambana na kutokomeza kundi hili. Zaidi ya nchi ishirini wanachama wa muungano huo zimeshiriki mkutano huo.

Kutoka kulia kwenda : Waziri mkuu wa Iraq, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Antony Blinken mwakilishi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika mkutano wamuungano wa kimataifa dhidi ya IS Juni 2,
Kutoka kulia kwenda : Waziri mkuu wa Iraq, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Antony Blinken mwakilishi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika mkutano wamuungano wa kimataifa dhidi ya IS Juni 2, REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao, viongozi wa nchi hizo wameunga mkono mpango uliyoandaliwa na Waziri mkuu wa Iraq Haidar al-Abadi ili kudhibiti upya mkoa wa al-Anbar.

Miezi tisa ya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za Islamic State, lakini mpaka sasa kundi hili bado linaonesha nguvu zake kwa kuendelea kuyateka baadhi ya maeneo nchini Iraq na Syria.

Muungano wa kimataifa unaoendesha vita dhidi ya Islamic State umeunga mkono mpango wa vitendo wenye lengo la kulidhibiti upya jimbo kubwa la Iraq la Al-Anbar, ambalo liko chini ya udhibiti wa wapiganaji wa Islamic State, ambo hivi karibuni wamedhibiti Ramadi, mji mkuu wa jimbo la Al-Anbar. Mpango huo unatazamiwa hususan kuunga mkono watu kutoka jamii ya Wasuni, ili waweze kushirikiana na jeshi la Iraq kwa kuendesha vita dhidi ya kundi hili lenye msimamo mkali la Daesh.

Katika tamko lao la mwisho, washiriki katika mkutano huo wa Jumanne Juni 2 pia wamekumbusha kuwa hali ya usalama imeendelea kuzorota nchini Syria. Kwa mujibu wa muungano huo, " Bashar Al Assad hana nia yakuendesha vita dhidi ya kundi hili ". Kwa hiyo " kunahitajika mchakato wa serikali ya mpito nchini Syria".

Viongozi hao kutoka zaidi ya nchi ishirini waliokutana Paris walisisitiza pia kuzingatia hali dharura ya kibinadamu inayoendelea kushuhudiwa nchini Iraq na Syria, na hivyo kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa kusaidia mamilioni ya wakimbizi waliokimbia makazi yao katika nchi hizo kutokana na machafuko yanayoendela.

Hatimaye tamko la mwisho pia linataja mali za mkoa huo, ambazo zinakabiliwa na vitisho, wakati ambapo wapiganaji wa Islamic State wamekua wakiudhibiti mji wa kale wa Palmyra, nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.