Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Shambulio la kigaidi laua waalimu watatu Kenya

Walimu watatu wameuawa baada ya watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al- Shabaab kuvamia kituo kinachotoa huduma mbalimbali cha Kamuthe katika jimbo la Garissa, Kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Askari wa Kenya baada ya shambulio la Al Shabab dhidi ya Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2015.
Askari wa Kenya baada ya shambulio la Al Shabab dhidi ya Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2015. CARL DE SOUZA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika shambulio hilo, wanamgambo hao pia waliharibu mtambo wa mawasiliano katika eneo hilo. polisi inaendelea kuwasaka magaidi hao, kwa mujibu wa chanzo cha polisi.

Viwango vya elimu katika jimbo la Garissa huenda vikashuka kutokana na mashambulizi ya magaidi kwenye eneo hilo.

Hii sio mara ya kwanza kwa walimu katika jimbo hilo la Garissa kuvamiwa na kuuwauwa. Miaka miwili iliyopita, walimu wawili waliuawa na kusababisha walimu wengine ambao hawakuwa wenyeji wa eneo hilo kukimbia kutoka eneo pana la kaskazini mashariki wakihofia usalama wa maisha yao.

Shambulio hilo linajiri wiki moja tu baada ya wanamgambo hao kushambulia shule ya msingi ya Saretho katika jimbo hilo la Garissa na kuwauwa wanafunzi wanne.

Hili ni shambulizi la 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi manne yalitokea Garissa, matatu Wajir, mawili Mandera na mawili mengine katika mji wa Lamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.