Pata taarifa kuu
KENYA-MAREKANI-Al SHABAB-USALAMA

Kenya: Wamarekani 3 miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio la Al Shabab

Idadi ya vifo kutokana na shambulio la Al Shabab dhidi ya kambi ya jeshi Mashariki mwa Kenya imeongezeka. Mapema Jumpili, mamlaka nchini Kenya ilisema magaidi 4 waliuawa na washukiwa 5 walikamatwa.

Afisa wa polisi ya Kenya katika kaunti ya Lamu, Januari 2, 2020. (picha ya kumbukumbu)
Afisa wa polisi ya Kenya katika kaunti ya Lamu, Januari 2, 2020. (picha ya kumbukumbu) © REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Jumapili jioni, Marekani kupitia makao yake ya kijeshi barani Afrika AFRICOM, ilikiri kwamba shambulio dhidi ya Kambi ya Simba liligharimu maisha ya raia watatu kutoka Marekani. Askari mmoja na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Ulinzi. Wafanyakazi wengine wawili wa wizara hiyo wamejeruhiwa na na sasa wanaendelea vizuri.

Wakati wa shambulio lao, wanamgambo wa Al Shabab walidai kuwa walitekeleza hasara kubwa kwa upande wa askari wa Marekani na Kenya walioko kwenye kambi hiyo.

Washington imekuwa ikishtumu kundi hilo la wanamgambo wa Kiislamu kutokusema ukweli kwa hali inayotokea ili kuendelea propaganda yao. Hata hiyo iliongeza kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini uharibifu huo. Mamlaka ya Kenya pia ilisema kwamba hakuna askari aliyejeruhiwa wala kuuawa katika shambulio hilo.

Marekani kupitia makao yake makuu ya jeshi barani Afrika, hatimaye, imekiri kupoteza baadhi ya raia wake katika shambulio hilo, huku ikibaini kwamba ndege sita pia zimeharibiwa.

"Tunaendelea kuwasaka waliohusika," ameahidi Jenerali Stephen Townsend, kamanda wa jeshi la Marekani barani Afrika, AFRICOM.

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia, lilivamiwa kambi ya kijeshi inayowatumiwa na wanajeshi wa Kenya na Marekani katika la Lamu, Pwani ya nchi hiyo.

Shambulizi hilo lililenga kambi hiyo inayoitwa Simba, katika eneo la Manda Bay.

Lamu ni kivutio cha utalii nchini Kenya lakini pia inapakana na nchi ya Somalia kupitia Bahari Hindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.