Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-MAREKANI-AL SHABAB

Al Shabab yashambulia kambi ya kijeshi inayotumiwa na Kenya na Marekani

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia, limevamiwa kambi ua kijeshi inayowatumiwa na wanajeshi wa Kenya na Marekani katika la Lamu, Pwani ya nchi hiyo.

Uwanja wa ndege wa Lamu, uliokuwa umefungwa kwa muda baada ya shambulizi hilo Januari 05 2019
Uwanja wa ndege wa Lamu, uliokuwa umefungwa kwa muda baada ya shambulizi hilo Januari 05 2019 REUTERS/Abdalla Barghash
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lililega kambi hiyo inayoitwa Simba, katika eneo la Manda Bay.

Lamu ni kivutio cha utalii nchini Kenya lakini pia inapakana na nchi ya Somalia kupitia Bahari Hindi.

Marekani kupitia makao yake ya kijeshi barani Afrika AFRICOM, imethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo ambalo kundi la Al Shabab limedai kuhusika.

Hata hivyo, Jeshi la Kenya limesema kuwa, lilifanikiwa kuwauwa magaidi wanne wa Al Shabab katika shambulizi hilo lilitokea Jumapili asubuhi.

Uwanja wa ndege wa Lamu, ulifungwa kwa kutokana na shambulizi hilo lakini baadaye ukafunguliwa tena baada ya hali kutulia katika eneo hilo ambalo ni kivutio kikubwa cha wataliii nchini humo.

Marekani imeendelea kutekeleza mashambulizi ya angaa kuwalenga Al Shabab nchini Somalia.

Mwshoni mwa mwaka 2019, ndege za kivita za Marekani zilitekeleza shambulizi lililowauwa washukiwa wanne wa Al Shabab, baada ya kundi hilo kutekeleza shambulizi mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya zaidi ya watu sabini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.