Pata taarifa kuu
KENYA

Chama cha Jubilee chafuta uteuzi wa wagombea katika kaunti zote

Chama tawala cha Jubilee nchini Kenya kimefutilia mbali shughuli za uteuzi wa wagombea wake katika kaunti zote hapo jana baada ya uchaguzi huo kukabiliwa na visa vya uchomaji wa vifaa vya kupigia kura, na mgomo wa wapiga kura. 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta  na mweyekiti wa chama tawala cha Jubilee
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mweyekiti wa chama tawala cha Jubilee REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amesema kuwa chama hicho kitatoa tarehe mpya za uchaguzi leo Jumamosi.

Kwa mujibu wa Tuju hapo awali alikuwa amesema kuwa baada ya mazungumzo na viongozi wakuu wa chama hicho ,ilikubaliwa kwamba uchaguzi huo uahirishwe hadi siku nyengine ili kuweka uwazi na usawa.

Wiki iliopita shughuli kama hiyo ilifanyika katika chama cha upinzani cha ODM kinachoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila odinga ambapo kulikuwa na ghasia katika maeneo ya magharibi mwa Kenya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.