Pata taarifa kuu
KENYA

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA haujaafikiana kuhusu mgombea urais

Mwafaka bado haujapatikana kati ya vigogo wanne wa kisiasa wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, kuhusu ni nani kati yao atapeperusha bendera ya muungano huo kupambana na rais Uhuru Kenyatta wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu.

Viongozi wa upinzani nchini Kenya Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga na Moses Wetangula
Viongozi wa upinzani nchini Kenya Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga na Moses Wetangula REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyovuja kutoka kwa watalaam waliopewa jukumu la kuusadia muungamo huo kumtafuta mgombea wa urais inapendekeza kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga awe mgombea urais, huku aliyekuwa Makamu wa rais Kalonzo Musyoka awe mgombea mwenza wake.

Wanasiasa wengine, Moses Wetangula na Musalia Mudavadi inaelezwa kuwa wamepangiwa nafasi zingine za juu ikiwa serikali ya NASA itafanikiwa kuingia madarakani.

Hata hivyo, wanasiasa hao wanasema hakuna mwafaka wowote ambao umeshafikiwa na bado mashauriano yanaendelea ili kumtafuta mgombea huyo.

"Nashangaa kuwa suala linaendelea kuwa gumzo katika vyombo vya Habari hapa nchini, hili ni suala letu mtuachie," alisema Raila Odinga.

"Tumekutana lakini hakuna mwafaka wowote uliofikiwa," Kalonzo Musyoka naye alinukuliwa akisema wiki hii.

Vyama vinavyounda muungano huo vinasisitiza kuwa, ni sharti mgombea wao apeperushe bendera ya muungano huo.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa huenda muungano huo ukamtaja mgombea wake kabla ya mwisho wa mwezi wa Aprili.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.