Pata taarifa kuu

DRC : EU yalaani shambulio la bomu kwenye kambi ya wakimbizi mjini Goma

Umoja wa Ulaya na wenyewe mwishoni mwa juma lililopita umejitokeza na kulaani kile ilichosema hakikubaliki, baada ya waasi wa M23, kurusha bomu lililoanguka katika kambi ya raia waliokimbia mapigano mashariki mwa nchi hiyo ya Mugunda jirani na mji wa Goma, ambapo watu zaidi ya 10 waliuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.

Watu zaidi ya 10 waliuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Watu zaidi ya 10 waliuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa katika shambulio hilo. AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu jumuiya ya SADC kupitia tume yake ya kulinda amani nchini DRC, SAMIDRC, nayo ikilaani kilichofanyika.

Tume ya ulinzi ya jumuiya hiyo, SAMIDRC, imethibitisha shambulio hilo kusababisha madhara, wengi kati yao wakiwa wanawake na watoto.

Katika tarifa yake, SAMIDRC imesema mashambulio yanayolenga raia kwa makusudi hayakubaliki na kwamba yanakiuka misingi ya sheria za kimataifa.

Mbali na SADC, shambulio hilo pia limekashifiwa na Marekani iliyoinyooshea kidole nchi jirani ya Rwanda kwa kuwasaidia waasi hao kutatiza usalama mashariki mwa Congo, tuhuma ambazo tayari Kigali imekanusha.

Wanajeshi wa SADC wanaendelea kupambana na makundi yenye silaha mashariki ya DRC.
Wanajeshi wa SADC wanaendelea kupambana na makundi yenye silaha mashariki ya DRC. REUTERS - ARLETTE BASHIZI

Tayari mamlaka jijini Kinshasa, imeitaja Rwanda waziwazi kuhusika kwenye shambulio hilo, huku ikitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya kile kilichofanywa na waasi hao.

Kundi la M23 limeendelea kutatiza usalama mashariki mwa nchi hiyo, licha ya uwepo wa vikosi vya SADC na vile vya umoja wa Mataifa, MONUSCO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.