Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Upinzani nchini Kenya waahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Januari 4

Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD, umesema umeahirisha maandamano yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe 4 mwezi Januari mwaka ujao, kupinga mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi.

Raila Odinga, Waziri mkuu wa zamani wa Kenya, ambaye ni kiongozi wa upinzani, Julai 7, 2014 mjini Nairobi.
Raila Odinga, Waziri mkuu wa zamani wa Kenya, ambaye ni kiongozi wa upinzani, Julai 7, 2014 mjini Nairobi. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada Kamati ya Senate kuanza mazungumzo kuhusu mabadiliko hayo yaliyofanywa na Bunge la kitaifa na kuwahusisha wadau mbalimbali wa Uchaguzi wakiwemo wananchi.

Jumatano wiki hii Maseneta nchini Kenya, walikubaliana kuwa mjadala wa mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi ushughulikiwe katika Kamati ya Haki za Binadamu na sheria.

Uamuzi huu ulikuja baada ya Maseneta kukutana kwa dharura kujadili mabadiliko hayo yaliyopitishwa na bunge la kitaifa wiki iliyopita na kuzua mjadala wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Mabadiliko hayo yanaipa nafasi Tume ya Uchaguzi kutumia njia mbadala ya kuwatambua na kujumuisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu ikiwa mfumo wa Ki-eletroniki utagoma siku ya kupiga kura.

Spika wa Baraza la Senate Ekwe Ethuro alisema, Kamati hiyo itatoa nafasi kwa mashirika ya kiraia, viongozi wa dini na wadau wengine kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko hayo.

“Waheshimiwa Maseneta, naagiza kuwa Kamati ya sheria na haki za binadamu ishughulikie mswada huu, kwa mujibu wa Katiba na kanuni zetu kuanzia hivi leo," alisema Bw Ethuro.

"Lakini pia naagiza kuwa Kamati hii iwahusishe wadau wote wa uchaguzi na wananchi na kuzingatia yale yote yanazunguziwa kuhusu mswada huu,” aliongeza Ekwe Ethuro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.