Pata taarifa kuu

Kenya: Miili ya baadhi ya waliofariki msituni Shakahola yakabidhiwa kwa familia

Nairobi – Mamlaka nchini Kenya, zinaendelea kukabidhi miili ya watu waliofariki kutokana na njaa baada ya kupokea maelekezo ya mchungaji mwenye utata Paul McKenzie, aliyewaagiza kufunga hadi kufa ili wakutane na Mungu, hatua hii inakuja ikiwa ni mwaka mmoja tangu kugunduliwa kwa makaburi ya pamoja kwenye msitu wa Shakahola, Pwani ya Kenya.

Zoezi hilo limeanza hapo jana ambapo miili saba ikikabididhiwa kwa família tatu kwa ajili ya mazishi
Zoezi hilo limeanza hapo jana ambapo miili saba ikikabididhiwa kwa família tatu kwa ajili ya mazishi REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo limeanza hapo jana ambapo miili saba ikikabididhiwa kwa família tatu kwa ajili ya mazishi baada ya kupewa ushauri wa kisaikolojia na wanachama wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu.

Hii inajiri baada ya Mchakato wa uchungu wa utambuzi  wa miili ambao umechukua mwaka, kwa sababu  ya miili mingi ilikuwa imeharibika, uwepo wa  idadi kubwa ya kesi, na  ukosefu wa  vifaa vya kufanya vipimo vyote vya vinasaba yaani DNA.

Katika ripoti iliyotolewa na tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadaam ,wiki iliyopita iliwalaumu maofisa wa serikali kwa kuzembea kazinui na kushindwa kuzuia mauaji hayo.

Tayari mchungaji Mackenzie ameshtakiwa kwa makosa ya ugaidi na mauaji  ya washirika wake, mashtaka ambayo hata hivyo amekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.