Pata taarifa kuu

Maelfu kadhaa ya waandamanaji kupinga mageuzi ya uchaguzi nchini Tanzania

Maelfu kadhaa ya watu wamekusanyika Jumatano katika mji mkuu wa uchumi wa Tanzania Dar es Salaam kwa wito wa chama kikuu cha upinzani kushutumu miswada mitatu ya mageuzi ya uchaguzi.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini mwezi Machi, 2023.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini mwezi Machi, 2023. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

 

Ni maandamano muhimu zaidi tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa ya upinzani mwezi Januari 2023 iliyotangazwa mwaka 2016 na mtangulizi wake John Magufuli.

 

Chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA kinapinga hasa nakala inayomruhusu mkuu wa nchi kuteua wajumbe watano kati ya 10 wa tume ya uchaguzi. Hapo awali, rais aliteua tume nzima.

 

Kiongozi wa chama cha upinzani cha CHADEMA, Freeman Mbowe, anasema mabadiliko yaliyopangwa ni “marekebisho ya sura” tu.

 

"Huu ni mwanzo tu," alisema mwanzoni mwa maandamano hayo, na kuthibitisha kwamba maandamano hayo yataenea katika mikoa mingine hadi mamlaka itakapokubali matakwa ya upinzani.

 

"Serikali ya Tanzania haiwasikilizi watu wake licha ya kwamba wanapitia wakati mgumu," ameongeza, akizungumzia hali ya uchumi ya nchi hii ya Afrika Mashariki iliyokumbwa na ongezeko la gharama ya maisha, ambapo asilimia 44 ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

 

Chini ya ulinzi mkali wa polisi, msafara wa rangi nyekundu, nyeupe na bluu wa chama cha CHADEMA ulianzia nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam hadi kufika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

 

"Tunataka kuiambia serikali kuondoa miswada ambayo kimsingi inalenga kulinda chama tawala," amesema Mdude Nyagali, muandamanaji kutoka Mbeya, kilomita 820 magharibi mwa Dar es Salaam.

 

"Tunahitaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi," imeandikwa kwenye moja ya mabango ya waandamanaji.

 

Akiingia madarakani mwezi Machi 2021 baada ya kifo cha ghafla cha kiongozi dikteta John Magufuli, Samia Suluhu Hassan alibatilisha baadhi ya hatua zinazozuia uhuru wa kisiasa na kuahidi mageuzi yaliyotakwa na upinzani kwa muda mrefu.

 

Hasa, aliidhinisha kuchapishwa kwa magazeti manne yaliyopigwa marufuku hapo awali, kuondoa marufuku ya mikutano ya upinzani na kuruhusu kurejea kwa Tundu Lissu, kiongozi wa upinzani Tanzania, kutoka uhamishoni kwa kipindi cha miaka mitano.

 

Mwezi Machi, Samia Suluhu Hassan alitangaza, wakati wa mkutano wa upinzani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Wanawake, kwamba anataka kurejesha "ushindani wa uchaguzi" na kuzindua upya mchakato wa marekebisho ya katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.