Pata taarifa kuu

Tanzania: Licha ya changamoto katika usawa wa jinsia, wanaharakati wameridhika na rais Samia

NAIROBI – Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hivi leo atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kihistoria nchini humo, ambapo atashiriki kwa mara ya kwanza mkutano wa baraza la wanawake wa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA wakati wa sherehe za siku ya wanawake duniani.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Hamasa kwa wanawake, Ijumaa ya Tarehe 19 Machi 2021 Samia Suluhu Hassan aliapishwa kuwa Rais wa nchi hii,rais wa kwanza mwanamke kushika madaraka makubwa, anaamini mwanamke ni chachu ya wanaweza.

“Huko Nyuma hatukuamini kama mwanamke anaweza kwa sababu niko kwenye maji ya moto nitafanya’ amesisitiza rais Samia Suluhu Hassan.

00:06

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Aida Kenaan ni Mbunge pekee wa kuchaguliwa kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA akiwakilisha jimbo la Nkasi kaskazini, anasema Rais samia kaonesha utofauti

kuhusu demokrasia ameeleza kuhusu maridhiano na majadiliano hiyo ni sifa ya kwanza, tumeona sasa ile dhana imeanza kuonekana kuwa kuna bunge kuna mahakama kuna serikali.’’ameelezaAida Kenaan.

00:06

Aida Kenaan ni Mbunge pekee wa kuchaguliwa kupitia chama cha CHADEMA

Changamoto gani zinamkabili Rais Samia, licha ya kupiga hatua? Anna Henga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini humu.

“Ukatili wa kijinsia bado upo juu sana hasa kwa wanawake, uwezeshaji wanawake kiuchumi bado haitoshi sana. ”amesemaAnna Henga.

00:13

Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania

Wanawake nchini humu wanazungumziaje utendaji wa rais Samia?

“Amefanikisha kama barabara, hosipitali kujengwa, shule na ni kiongozi ambaye anawasikiliza watu.”Wamesema baadhi ya wanawake nchini humo.

00:08

Maoni ya wanawake nchini Tanzania kuhusu uongozi wa rais Samia

Wanawake wameongezeka katika nafasi za juu za uteuzi ikiwa ni pamoja na katika Baraza la mawaziri,akiwateua kuongoza wizara nyeti zikiwemo ya ulinzi na mambo ya nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.