Pata taarifa kuu
SIASA-MARIDHIANO

Tanzania: Rais Samia Suluhu Hassan anataka 'kuandika ukurasa mpya' na upinzani

Siku ya Haki za Wanawake iliadhimishwa, Jumatano, Machi 8, na ushiriki wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kongamano la upinzani. Akiwa amealikwa na Umoja wa Wanawake wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani mkoani Kilimanjaro, mkuu huyo wa nchi aliahidi “kuandika ukurasa mpya” pamoja na waliokuwa wapinzani wake, akivunja ubabe wa mtangulizi wake.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Aprili 15, 2022 mjini Washington.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Aprili 15, 2022 mjini Washington. AP - Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Vilio vya furaha na ngoma za kumkaribisha mgeni wa heshima, vilitawala ukumbi huo, ikiwa ni jambo la nadra huonekana katika safu ya upinzani. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alifika Jumatano, Machi 8, katika ukumbi uliojaa watu, kuwasilisha ujumbe wa maridhiano:

“Leo tunaandika historia mpya ambayo itaunganisha nchi yetu. Ukweli kwamba niko hapa leo ni ishara ya mabadiliko ninayoyatekeleza. Mabadiliko yanaendelea na tutajenga nchi mpya, kwa kuzingatia ushindani mzuri kati ya vyama vya siasa, na bila vurugu. "

Katika hadhara hiyo kiongozi wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe alikuwepo. Rais Samia Suluhu Hassan alimfanya mwanasiasa huyo akamatwe mnamo 2021 kwa ugaidi, kabla ya kumwachilia miezi saba baadaye. Leo mahusiano yao yako vizuri, lakini bado kuna maswali ya kuudhi hasa Bungeni. Tangu mwaka 2020, chama tawala kimekuwa kikidaiwa kuwashawishi wabunge 19 kutoka Chadema kushiriki vikao vya bunge kwa niaba ya upinzani. Na hili bila kibali cha rais wao, Freeman Mbowe, ambaye alisema:

“Ukweli wa kuwatuma wabunge 19 kuketi Bungeni bila ridhaa ya chama chetu ni kinyume cha Katiba. Hawa wanawake hatuwapingi, waliwahi kuwa viongozi wetu, lakini wamerubuniwa, na waliosaidia hawa wabunge kuvunja sheria ni sehemu ya serikali yako. Mheshimiwa rais, suala hili linatusumbua sana. "

Uwepo wa wabunge hao 19 ulimwezesha Rais wa zamani, John Magafuli, kufuta sura ya Bunge la chama kimoja, wakati upinzani haukupata kiti hata kimoja katika uchaguzi uliopita wa wabunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.