Pata taarifa kuu

Tanzania: Tutarejesha siasa zenye ushindani: Rais Samia

NAIROBI – Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake itahakikisha inarejesha siasa zenye ushindani huku akisisitiza kuwa hivi karibuni mchakato wa kuelekea kupata katiba mpya utaanza, hili likiwa dai la muda mrefu la vyala vya upinzani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA © Tanzania State House
Matangazo ya kibiashara

Rais Samia alisema haya alipohudhuria kongamano la wanawake wa chama kikuu cha upinzani Chadema.

“Kuwepo hapa ni moja kati ya hayo mageuzi, kila safari ya maendeleo huaanza na hatua, hatuwezi kuwa tumezungumza juzi na leo kila kitu kiwe kiko tayari.”amesema rais Samia.

 

00:32

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

 

Aidha mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alimtaka rais Samia kulitazamla suala la wabunge 19 waliofukuzwa na chama chao lakini wanaendelea kuwepo bungeni.

“Kitendo cha kuwapeleka wabunge 19 ndani ya bunge ambao hawakutokana na uamuzi wetu wa chama ni uvunjaji wa katiba na sheria na ni uhuni ambao haupaswi kuvumiliwa na mpenda haki.”amesisitiza Freeman Mbowe.

 

00:29

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama cha Chadema nchini Tanzania

 

Siku ya Jumatano ya wiki hii rais Samia aliweka historia ya kuwa rais wa kwanza aliyeko madarakani kuhudhuria kongamano la chama kikuu cha upinzani.

Vyama vya kisiasa vya upinzani nchini Tanzania vinaendelea na kufanya mikutano ya kisiasa baada ya rais Samia kutangaza kuondoa marafuko iliyotangazwa na mtangulizi wake hayati John Pombe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.