Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-SIASA

Kenya: Matumaini ya kufanyika kwa mazungumzo yafifia baada ya miezi kadhaa ya maandamano

Wakaazi wa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, walitarajia Jumatano kufanyika kwa mazungumzo kati ya rais na upinzani, ambao walisema wako tayari kuzungumza baada ya miezi kadhaa ya maandamano mabaya dhidi ya serikali na kupanda kwa gharama ya maisha.

Wito wa utulivu na mazungumzo umeongezeka katika wiki iliyopita kutoka kwa Umoja wa Mataifa, nchi za Magharibi na makasisi na vyombo vya habari vya Kenya.
Wito wa utulivu na mazungumzo umeongezeka katika wiki iliyopita kutoka kwa Umoja wa Mataifa, nchi za Magharibi na makasisi na vyombo vya habari vya Kenya. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne jioni, Mkuu wa Nchi William Ruto alikariri kwamba "yuko tayari (...) kukutana" na kiongozi wa upinzani Raila Odinga baada ya kiongozi huyo kusema "yuko tayari (...) kwa mazungumzo kwa wakati wowote".

Jaribio la hapo awali la majadiliano kati ya kambi hizo mbili, lililoanzishwa baada ya maandamano ya kwanza yaliyoandaliwa na upinzani mwezi Machi, kushindwa, na kusababisha kuanza tena mapema mwezi Julai kwa maandamano mapya ambayo yaligubikwa na uporaji, vitendo vya uharibifu na makabilinao mabaya na polisi. 

"Wakae chini wazungumze. (...) Wasipozungumza wao kwa wao, mkwamo hautaisha na mateso yetu yataendelea", amesema Josphat Ng'atho, 36, dereva wa "boda boda" (pikipiki ya kukodiwa ).

"Nionyeshe mtu ambaye hajachoshwa na maandamano," amesema Cate Wafula, 29, mhudumu wa mapokezi katika jengo la ofisi. “Siji kazini kila kunapokuwa na maandamano kwa sababu naogopa kuvamiwa na kuibiwa,” ameongeza.

Wito wa utulivu na mazungumzo umeongezeka katika wiki iliyopita kutoka kwa Umoja wa Mataifa, nchi za Magharibi na makasisi na vyombo vya habari vya Kenya. Kulingana na muungano wa upinzani Azimio, takriban watu 50 wameuawa tangu mwezi Machi - karibu ishirini, kulingana na takwimu rasmi - katika kipindi cha siku tisa za kwanza za maandamano.

Siku ya kumi iliyopangwa kufanyika Jumatano imegeuzwa kuwa heshima kwa "wahanga wa ghasia za polisi", kwa "gwaride na mikesha ya mshikamano". "Tunatoa wito kwa Wakenya kujitokeza, kuwasha mishumaa na kuweka maua" katika kumbukumbu yao, muungano wa upinzani Azimio umesema katika taarifa

Upinzani ulitangaza kusitisha maandamano kuwakumbuka wafuasi wake waliouawa wakati wa maandamano
Upinzani ulitangaza kusitisha maandamano kuwakumbuka wafuasi wake waliouawa wakati wa maandamano © Gladys Wanga- Gavana Homabay
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.