Mkosoaji wa Kagame, Rwigara atangaza kuwania katika kinyang'anyiro cha urais
Shima Diane Rwigara, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa uongozi wa rais wa Rwanda Paul Kagame, ametangaza kuwa atawania urais wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Julai.
Imechapishwa:
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, Rwigara, amesema anafungua ukurasa mpya kwenye uwanja wa kisiasa na kuwaomba Wanyarwanda wamuunge mkono ili kuandikisha historia.
A new chapter for Rwanda begins now.
— Shima Diane Rwigara (@ShimaRwigara) May 8, 2024
Together we will make history!
Join me as I run for President.#RwandaElections2024
Twagiye…
Rwigara, mwenye umri wa miaka 42, ni kiongozi wa chama cha People Salvation Movement, alikuwa awanie uchaguzi wa mwaka 2017 lakini hakuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi.
Wakati huo, baada ya tangazo lake, picha zake za utupu ziliwekwa mtandao, katika kile alichokisema kuwa, alilengwa kisiasa ili kumyamazisha.
Hapo nyuma, aliwahi pia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kughusi nyaraka na uchochezi dhidi ya serikali ya rais Kagame.
Mbali na Rwigara, rais Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2000, anatarajiwa kuùenyana na wagombea wengine wawili Frank Habineza kutoka chama cha Green na mgombea binafsi Philippe Mpayimana, kwenue uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mwezi Julai, anaotarajiwa kushinda.