Kenya: Maombi ya kuwakumbuka waliofariki katika maandamano yamefanyika
Nairobi – Nchini Kenya, wakaazi katika baadhi ya maeneo yakiwemo Kisii, Magharibi ya Kenya, Nairobi na Mombasa pwani ya taifa hilo la Afrika Mashariki , leo Jumatano wamewasha mishumaa na kufanya maombi kwa ukumbusho wa Wakenya waliofaririki wakati wa maandamani ya upinzani kulaani kupanda kwa gharama ya maisha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hatua hii inakuja baada ya upinzani nchini humo kutangaza kusitisha maandamano yaliokuwa yamepangwa kufanyiak juma hili.
“Tumekuja kuwasha mishumaa kuwakumbuka watu waliofariki baada ya kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano dhidi ya serikali. Pia tungependa kuwakumbusha polisi kwamba hatuna shida nao bali tunatekeleza haki yetu ya kikatiba pekee,” mmoja wa wakaazi wa Kisii, Magharibi ya Kenya amesema.
Kisii residents light candles in memory of lives lost during anti-government protests pic.twitter.com/HAxWQxvQWi
— NTV Kenya (@ntvkenya) July 26, 2023
Katika taarifa iliyotolewa na Muungano wa Azimio (Upinzani) Julai 25, wananchi katika maeneo mbalimbali nchini humo wametakiwa kuwasha mishumaa na kuweka maua katika maeneo mbalimbali ya makutano yakiwemo ya mbuga, hospitali, vituo vya mabasi na makanisa ili kuonyesha upendo na heshima yao kwa wahanga wa maandamano dhidi ya serikali.
Katika taarifa nyingine ya Julai 24, upinzani ulisema kwamba "nchi kwa sasa inakabiliwa na hali isiyokuwa ya kawaida ya ukatili wa polisi, na Serikali inawatumia watu wenye silaha ili kuzima maandamano."
Tume ya kitaifa ya haki za binadamu katika taifa hilo pia ililaani vitendo vya ukatili wa polisi vilivyosababisha watu kupoteza maisha wakati wa maandamano, madai ambayo wizara ya usalama wa ndani inaendelea kukanusha.
Mnamo Jumanne, Julai 25, katibu mkuu katika wizara ya mambo ya ndani na kitaifa Raymond Omollo alitangaza kwamba afisa sheria mmoja wa polisi aliuawa na wengine 305 kujeruhiwa wakati wa maandamano ya Azimio.
Raila Odinga visits Kenyans who were injured during anti-government protests
— NTV Kenya (@ntvkenya) July 26, 2023
Via @SChazima pic.twitter.com/CAiUNaZAxL
Kwa upande mwengine viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, wametembelea baadhi ya wafuasi wao waliojeruhiwa ambao wamelazwa katika hosipitali tofauti jijini Nairobi.