Pata taarifa kuu

DRC: Ripoti ya UN inasema ukiukaji wa haki za binadamu umepungua

Ofisi ya pamoja ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa na Serikali ya Congo, imesema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vimepungua kwa asilimia tano nchini DRC tangu mwezi Machi mwaka huu.

Makundi ya watu wenye silaha yamekuwa yakilaumiwa kwa kuchangia pakubwa katika visa vya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuwateka raia mashariki ya nchi.
Makundi ya watu wenye silaha yamekuwa yakilaumiwa kwa kuchangia pakubwa katika visa vya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuwateka raia mashariki ya nchi. © Alexis Huguet, AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, ofisi hiyo pia imeeleza kupungua kwa asilimia zaidi ya 18 kwa wahanga wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika maeneo mengi ya taifa hilo, ambapo ilirekodi matukio 360 pekee ukilinganisha na miezi iliyopita.

Kwa mujibu wa wataalamu kwenye ofisi hiyo, wamesema kupungua kwa matukio hayo, kumetokana na rekodi ndogo ya idadi ya waathiriwa wa mauaji, unyanyasaji na utekaji unaofanywa na makundi yenye silaha katika majimbo yanayoshuhudia utovu wa usalama.

Aidha wataalamu hao wamesema tofauti na rekodi zilizopita, idara za usalama za Serikali zimehusika katika matukio 176 ya ukiukaji wa haki za bindamu ikiwa ni ongezeko la asilimia 49 kutoka 42, huku makundi yenye silaha yalihusika na vitendoi 174.

Ripoti hii inakuja wakati huu serikali ya Kinshasa ikiendelea kuimarisha vita dhidi ya makundi ya waasi mashariki ya DRC kwa ushirikiano na vikosi vya SADC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.