Pata taarifa kuu

IMF na DRC zinakaribia kuafikia makubaliano ya mkopo kwa Kinshasa

Mamlaka za DRC zinakaribia kufikia makubaliano na shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu nchi hiyo kupatiwa mkopo utakaoisaidia kukabiliana na changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na athari za uviko 19 pamoja na utovu wa usalama mashariki mwa nchi hiyo.

Mamlaka za DRC zinakaribia kufikia makubaliano na shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu nchi hiyo kupatiwa mkopo
Mamlaka za DRC zinakaribia kufikia makubaliano na shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu nchi hiyo kupatiwa mkopo REUTERS - Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa sasa, DRC imekuwa katika majadiliano na IMF kuhusu uwezekano wa kupatiwa usaidizi wa kifedha, Kinshasa ikisifiwa kwa kufanikiwa kuandaa kwa amani uchaguzi wa mwaka uliopita pamoja na marekebisho ya sera zake za kiuchumi.

Hata hivyo licha ya hatua hizi, waangalizi wa IMF wanaitaka Serikali ya Congo kufanya zaidi katika kuongeza vyanzo vya mapato pamoja na ubanaji wa matumizi utakaowezesha kuimarika kwa uchumi Wake.

Aidha IMF inaitaka Kinshasa, kudhibiti matumizi ya fedha za uma, kurekebisha sera za kifedha na kuimarisha masuala ya utawala bora na taasisi za uma.

Akizungumza na wanahabari mwezi uliopita, waziri wa fedha Nicolas Kazadi, alisema nchi yake imeongeza mapato ya nje hadi kufikia dola za marekani bilioni 5 pamoja na kuongeza uwekezaji wa nje, jambo lililogusiwa pia na rais Felix Tshisekedi katika ziara yake ya hivi karibuni kwenye nchi za Ujerumani na Ufaransa .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.