Pata taarifa kuu

Ebola: Uganda yapokea dozi mpya za majaribio za chanjo

Uganda imetangaza Alhamisi kuwa imepokea shehena ya chanjo mbili ili kupima ufanisi wake dhidi ya ugonjwa wa Ebola ambao umesababisha vifo vya makumi ya watu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Mhudumu wa afya akinyunyuzia dawa inayotumiwa kwa wagonjwa wa Ebola katika kituo cha Afya cha Madudu III, wilayani Mubende, Uganda.
Mhudumu wa afya akinyunyuzia dawa inayotumiwa kwa wagonjwa wa Ebola katika kituo cha Afya cha Madudu III, wilayani Mubende, Uganda. AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

Tangu mamlaka ilipotangaza mlipuko wa Ebola Septemba 20, nchi hiyo imerekodi visa 142 vilivyothibitishwa na vifo 56. Kuenea kwa virusi hivyo kumepungua katika wiki za hivi karibuni, hata hivyo, na kuongeza matumaini kwamba ugonjwa huo unaweza kutokomezwa.

Hii ilisababishwa na virusi vya Ebola aina ya Sudan, ambayo kwa sasa hakuna chanjo. Lakini chanjo tatu za majaribio, moja iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na Taasisi ya Jenner huko Uingereza, nyingine iliyotengenezwa na Taasisi ya Sabin Vaccine nchini Marekani na ya tatu iliyotengenezwa na Mpango wa Kimataifa wa Chanjo ya UKIMWI (IAVI) zitafanyiwa majaribio nchini Uganda katika wiki zijazo.

Mnamo Desemba 8, Uganda ilipokea shehena yake ya kwanza ya dozi kutoka Taasisi ya Sabin Vaccine. "Jumamosi tarehe 17 Desemba, tulipokea chanjo mbili zaidi, dozi 2160 kutoka Merck/IAVI na dozi 2000 kutoka Chuo Kikuu cha Oxford/Jenner Institute iliyotengenzwa na Serum Institute of India, " Waziri wa Afya Jane Ruth Aceng amesema siku ay Alhamisi, wakati wa mkutano mkutano na waandishi wa habari.

Chanjo hizi zitapimwa kwa wagonjwa waliothibitishwa wa Ebola, pamoja na watu waliotangamana katika viwango viwili vya ukaribu. Mamlaka ya Uganda ilibainisha mwezi uliopita kwamba kesi mpya zilikuwa zikipungua na mgonjwa wa mwisho aliyethibitishwa na ugonjwa huo aliruhusiwa kutoka hospitali mnamo Novemba 30.

Kutokuwepo kwa visa vya ugonjwa wa Ebola katika siku za hivi karibuni kumechelewesha utekelezaji wa vipimo vya chanjo, kulingana na wataalam wa afya wa kimataifa wanaofanya kazi nchini Uganda. Lakini Jane Ruth Aceng amesema mamlaka tayari imeanza kuajiri watu wa kujitolea kwa ajili ya vipimo hivyo, akiongeza kuwa Uganda itahudhuria mkutano wa kimataifa wa mashauriano ya wataalamu kuhusu Ebola Januari 12.

Serikali wiki iliyopita iliondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa kwa miezi miwili kwa maeneo mawili yaliyoambukizwa, ikiwa ni pamoja na sheria ya kutotoka nje jioni hadi alfajiri, marufuku ya kusafiri, na kufungwa kwa masoko, baa na makanisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.