Pata taarifa kuu

Ebola yaua watu wengine saba Uganda

Wizara ya Afya nchini  Uganda imethibitisha vifo vya watu 7 vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya Ebola. Vifo hivyo vinaelezwa vimetokea katika kipindi cha siku mbili zilizopita. 

Taarifa ya wizara ya Afya  inasema wagonjwa wapya wanne wamethibitishwa kuambukizwa na kufanya jumla ya wagonjwa 48, Kati ya hao 14 bado wako hospitalini na 14 wamepona.
Taarifa ya wizara ya Afya inasema wagonjwa wapya wanne wamethibitishwa kuambukizwa na kufanya jumla ya wagonjwa 48, Kati ya hao 14 bado wako hospitalini na 14 wamepona. REUTERS/Edward Echwalu
Matangazo ya kibiashara

Vifo vya watu hawa saba kwa muda wa siku mbili,ndiyo idadi kubwa zaidi ambayo imeripotiwa na wizira ya afya tangu mlipuko wa Ebola kuthibitishwa mwezi uliopita  

Taarifa ya wizara inasema wagonjwa wapya wanne wamethibitishwa kuambukizwa na kufanya jumla ya wagonjwa 48, Kati ya hao 14 bado wako hospitalini na 14 wamepona.  

Katika hatua nyingine wahudumu wa afya wameeleza kuridhishwa na hatua ambazo serikali imechukua tangu watoe malalamiko yao kuhusu vifaa Kinga, lakini hata hivyo mwenyekiti wa chama cha madaktari Dkt Samuel Oledo, anasema ni lazima nchi ijiandae kwa wakati mgumu.  

Wakati wizara ya afya ikithibitisha vifo vya watu 17, shirika la afya duniani linasema watu 29 ndio wemefariki dunia tangu kulipuka kwa ugonjwa huo, miongoni mwao wapo watu wanaohisiwa kuwa walikuwa na maambukizo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.