Pata taarifa kuu
TANZANIA-UHURU

Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya uhuru wake

Tanzania bara zamani ikifahamika kama Tanganyika inaadhimisha miaka 60 ya uhuru hivi leo, baada ya kupata uhuru huo kutoka kwa wakolini Waingereza.

Mkutano kati ya Mao Tse-tung na mwasisi wa uhuru na rais wa Tanzania Julius Nyerere wakati wa ziara yake huko Beijing mnamo 1968.
Mkutano kati ya Mao Tse-tung na mwasisi wa uhuru na rais wa Tanzania Julius Nyerere wakati wa ziara yake huko Beijing mnamo 1968. Keystone-France\Gamma-Rapho via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Wakati, Tanzania ikiadhimisha miaka 60 ya uhuru, wananchi wa taifa hilo wamezungumzia kuhusu hali ya nchi yao na kutaka changamoto zinazowakumba kupewa suluhu.

Usiku wa kuamkia leo, rais Samia Suluhu Hassan, aliwahotubia raia wa nchi hiyo na kuelezea hatua zilizopigwa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru.

Mapambano ya uhuru Tanganyika ni yale yaliyofanyika katika Tanzania bara ya leo dhidi ya ukoloni.Tanganyika, kama nchi yenye mipaka maalumu, ilianzishwa baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, ilipokuwa chini ya mamlaka ya Uingereza.

Kabla ya hapo ilikuwa sehemu ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, pamoja na nchi za leo Rwanda na Burundi.

Baada ya kuvamiwa na majeshi ya wapinzani wa Ujerumani wakati wa vita, Shirikisho la Mataifa lilikabidhi sehemu kubwa ya makoloni ya Kijerumani kwa Uingereza na nchi nyingine kama "eneo la kudhaminiwa". Serikali ya Uingereza iliamua kutumia jina "Tanganyika" kufuatana na jina la ziwa kubwa kwenye mashariki ya eneo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.