Pata taarifa kuu
TANZANIA-UHURU

Mfahamu Kambarage Nyerere, mtetezi wa uhuru wa Tanganyika

Tanzania wiki hii inaadhimisha miaka 60, tangu ilipopata uhuru wake. Kilele cha maadhimosho haya, itakuwa ni Tarehe 9 mwezi huu. Lakini je, Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo alikuwa nani ?

Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere
Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere Butiama Gallery/Govt
Matangazo ya kibiashara

Nyerere alikuwa kiongozi wa Tanzania, na kabla ya hapo Tanganyika, baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1961, wakati huo ikifahamiaka kama Tanganyika kabla ya kuungana na Zanzibar mwaka 1964.

Anatambuliwa na Watanzania kama Baba wa Taifa, na aliongoza taifa hilo kubwa la Afrika Mashariki tangu uhuru, hadi kifo chake mwaka 1985.

Alifahamika kwa jina la Mwalimu, kufuatia taaluma yake kabla ya kujiunga na kujiunga na harakati za ukombozi na kupigania uhuru wa nchi yake kutoka kwa wakoloni.

Nyerere alikuwa katika mstari wa mbele wa kuunda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), na Tanganyika ilipopewa serikali 1960 na wakolini, alikuwa Waziri kiongozi na kuiongoza nchi yake hadi kupata uhuru mwaka mmoja baadaye mwaka 1961 na kuwa Waziri Mkuu wa kwanza.

Wakati wa uhai wake, anakumbukwa na Watanzania kwa mengi hasa kutumia lugha ya Kiswahili kuliunganisha taifa hilo, lakini haraka za serikali yake kuyasaidia mataifa ya Kusini mwa Afrika kupata uhuru, miongoni mwa mengine mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.