Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Tundu Lissu, amezindua kitabu chake jijini Nairobi nchini Kenya ijumaa ya juni 25,

Mwanasiasa wa upinzani wa Tanzania, Tundu Lissu, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji, hivi leo amezindua kitabu chake jijini Nairobi nchini Kenya, kitabu ambacho amegusia masuala ya utawala bora na kuingiliwa kwa muhimili wa bunge na Serikali.

Mwanasiasa wa upinzani wa Tanzania Tundu Lisu akiweka saini yake katika Kitabu alichozindua jijini Nairobi Kenya Juni 25 2021
Mwanasiasa wa upinzani wa Tanzania Tundu Lisu akiweka saini yake katika Kitabu alichozindua jijini Nairobi Kenya Juni 25 2021 © RFI Kiswahili-Hilary Ingaty
Matangazo ya kibiashara

Tundu Lissu, ambaye alikimbilia Ubelgiji, baada ya kunusurika kuuawa mwaka 2017 nchini mwake wakati akiwa bungeni, amezikosoa serikali za ukanda kwa kuingilia uhuru wa mabunge ya nchi hizo na kupitisha sheria gandamizi.

Haya yanajiri wakati mahakama kuu ya Tanzania leo imebatilisha hukumu ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, dhidi ya viongozi tisa wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema nchini humo.

Viongozi hawa ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe walikabiliwa na makosa 12 kati ya 13 ambayo walishtakiwa na mahakama ya Kisutu huko Daresalaam kwamba waliitisha maandamano bila kupewa kibali na kusababisha vurugu huku Freeman Mbowe pamoja na viongozi wenzake walitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 350 za kitanzania sawa na dola elfu kumi na tatu, lakini sasa baada ya kukata rufaa sasa mahakama kuu imeamuru kurejeshwa kwa fedha hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.