Pata taarifa kuu
TANZANIA-COVID 19

Tanzania yatoa tahadhari ya wimbi la tatu ya maambukizi ya Covid 19

Serikali ya Tanzania, imetoa tahadhari nyingine kwa raia wake kuhusu uwezekano wa taifa hilo kukumbwa na mlipuko wa tatu wa Covid 19, wakati huu mataifa jirani yakiripoti ongezeko la wagonjwa.

Afisa wa afya nchini Tanzania
Afisa wa afya nchini Tanzania © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika tarifa iliyotolewa na wizara ya afya nchini humo, imewataka raia kuchukua tahadhari za hali ya juu ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara pamoja na kuvaa barakoa kwenye maeneo ya uma.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wataalamu wamebaini kuwepo viashiria vyote vya kutokea mlipuko watatu wa maambukizi ya Covidi 19 kwenye taifa hilo, ambapo wizara imewataka raia kuwa makini.

Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa kwenye wizara ya afya nchini tanzania, Dr Leonard Subi, amesema nchi yao inaendelea kufuatilia mwenendo wa maambukizi hayo ndani na katika mataifa jirani, ambayo yameripoti ongezeko la wagonjwa.

Tangu aingie madarakani miezi michache iliyopita, rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alitangaza mikakati ya nchi yake kudhibiti kuenea kwa maambukizi hayo, ambapo aliunda tume ya wataalamu inayomshauri kuhusu ugonjwa huo.

Majuma kadhaa yaliyopita, rais Samia aliruhusu kuagizwa kwa chanjo za ugonjwa huo, hatua ambayo mwaka mmoja uliopita hakuna aliyeamini Tanzania inaweza kuchukua msimamo tofauti baada ya awali kupinga uwepo wa maambukizi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.