Pata taarifa kuu

Tanzania: Waziri wa afya awashauri wananchi kuvalia barakoa kwenye maeneo ya mikusanyiko

Waziri wa afya nchini Tanzania, Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuvaa barakoa wanapokuwa katika maeneo yenye watu wengi, ili kuzuia maambukizi ya vírus vya Corona.

Mwanamke anapita maandishi yaliyochorwa na wasanii kutoka kundi la Wachata ili kuongeza uelewa juu ya kuvaa barakoa kupambana na Covid-19, jijini Dar es Salaam, Mei 262020.
Mwanamke anapita maandishi yaliyochorwa na wasanii kutoka kundi la Wachata ili kuongeza uelewa juu ya kuvaa barakoa kupambana na Covid-19, jijini Dar es Salaam, Mei 262020. AFP - ERICKY BONIPHACE
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima  imeagiza wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona kwa kuvaa barakoa sehemu zenye mikusanyiko, ili kujikinga na wimbi la tatu lililoibuka katika mataifa mbalimbali.

aliagiza pia wananchi kuchukua tahadhari kwa kurejesha utaratibu wa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na matumizi ya vitakasa mikono ‘sanitizer’.

Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na kwamba inapokea wageni wengi kutoka nchi mbalimbali.

Tangu kuingia madarakani mwezi Machi, rais Samia Suluhu Hassan amebadilisha namna ya kukabiliana na janga la Corona kwa kuunda Kamati ambayo ilishauri matumizi ya chanjo na raia wa nchi hiyo kutumia mbinu zote za Kisayansi za kukabiliana na virusi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.