Pata taarifa kuu

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine waachiwa huru

Nchini Uganda, wanaharakati 18 kutoka chama cha Bobi Wine, wakiwemo watatu wa karibu sana na mpinzani huyo, waliachiliwa kwa dhamana Jumatatu, Juni 14, baada ya karibu miezi sita gerezani. Walikamatwa wakati wa kampeni za uchaguzi Desemba iliyopita, upinzani na vikundi vingi vya haki za binadamu vilitaka waachiliwe.

Mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine, na mlinzi wake, ambaye ameachiliwa tu baada ya karibu miezi sita kizuizini.
Mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine, na mlinzi wake, ambaye ameachiliwa tu baada ya karibu miezi sita kizuizini. REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amewakaribisha uraiani wanaharakati kumi na nane walioachiliwa kwa dhamana katika makao makuu ya chama chake Jumatatu. Miongoni mwao, Dan Magic, mtayarishaji wa muziki wa mwimbaji huyo aliyegeuka kuwa mpinzani, Nubian Li, msanii anayejulikana kwa kujitolea kwake, na Eddie Mutwe, mlinzi wa kibinafsi wa Bobi Wine.

Wanaharakati hao walikamatwa Desemba 30 mwaka jana wakati wa mkutano uliokuwa na hamasa kubwa sana, wakati mpinzani alizingirwa na vikosi vya polisi kabla ya kupelekwa hadi nyumbani kwake. Walishtakiwa mwanzoni kwa kutotii vizuizi vilivyohusishwa na janga la Covid-19, kisha walihamishiwa katika mahakama ya kijeshi mwezi Januari kwa makosa ya  kupatikana na risasi kinyume cha sheria. Bobi Wine alikaribisha kuachiliwa huku kwa dhamana, akiwashukuru Waganda ambao walijiunga kupinga kifungo chao.

Wajumbe wengi wa upinzani walikuwa wamekamatwa wakati wa kipindi cha uchaguzi: Wizara ya Mambo ya Ndani ilikiri mwezi Aprili mbele ya bunge kwamba ilikamata zaidi ya watu 1,000 wakati wa kampeni za uchaguzi Januari iliopita

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.