Pata taarifa kuu
MEXICO

Maelfu waandamana Mexico dhidi ya ushindi wa Enrique Pena Nieto

Maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu nchini Mexico wamejitokeza kupinga ushindi wa kiti cha uraisi ulioenda kwa Enrique Pena Nieto kwa tuhuma kuwa chama CHA PRI kilijihusisha na ununuaji wa kura jambo ambalo ni kinyume na sheria za uchaguzi.

Maaandamano yamefanyika nchini Mexico kupinga ushindi wake,Enrique Pena Nieto
Maaandamano yamefanyika nchini Mexico kupinga ushindi wake,Enrique Pena Nieto REUTERS/Tomas Bravo
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalikuwa yakipinga na kulaani ushindi wa kununua kura baada ya mgombea wa chama cha PRI Pena Nieto kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume na taratibu za uchaguzi.

Waandamanji hao walipaza sauti wakimtaka Pena kujiondoa na kuhamasishana kwa kutumia kauli mbiu isemayo Mexico bila Pena,Mexico bila PRI.
 

Maandamano hayo yanakuja wakati ni siku kadhaa zimepita tangu kutangazwa kwa ushindi wa Enrique Pena Nieto ambaye aligombea kiti cha uraisi kwa tiketi ya chama cha PRI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.