Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Canada: Kumi wauawa katika mashambulizi ya visu huko Saskatchewan

Watu kumi waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Jumapili katika mashambulizi ya visu katika jamii mbili huko Saskatchewan, nchini Canada, polisi imesema. Msako mkali umeanzishwa katika mikoa mitatu ili kuwapata washukiwa wawili.

Maafisa wa uchunguzi wanakusanyika karibu na eneo la tukio huko Weldon, Saskatchewan, Jumapili, Septemba 4, 2022.
Maafisa wa uchunguzi wanakusanyika karibu na eneo la tukio huko Weldon, Saskatchewan, Jumapili, Septemba 4, 2022. AP - Heywood Yu
Matangazo ya kibiashara

Ikijibu simu za dharura, polisi imepata miili kumi katika jamii ya wazawa ya James Smith Cree Nation na katika mji  jirani wa Weldon, Saskatchewan (Mkoa wa Magharibi), Naibu Kamishna wa Polisi Rhonda Blackmore amesema.

"Waathiriwa wengine kadhaa walijeruhiwa, 15 kati yao hadi sasa wamesafirishwa hadi hospitali mbalimbali," ameongeza, akiongeza kwamba polisi walikuwa wakiwatafuta "washukiwa wawili" na kuchunguza "matukio mengi ya uhalifu".

Yote yalianza mapema Jumapili asubuhi, ameripoti mwandishi wetu katika mjiw Quebec, Pascale Guéricolas.

Washukiwa hao wametambuliwa, wanaume wawili kwa majina Damien Sanderson na Myles Sanderson, wenye umri wa miaka 30 na 31, wenye nywele nyeusi na macho ya kahawia. Inasemekana kwamba baada ya uhalifu huo waliondoka kwa gari nyeusi aina ya Nissan Rogue, Bi Blackmore alisema. Vikosi vya polisi vilitumwa kuwakamata.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.