Pata taarifa kuu

Vurugu mpya nchini Mexico: Miili mingine imepatikana kaskazini mwa nchi

Miili tisa ilipatikana Jumatano, Mei 8, katika mji wa kaskazini mwa Mexico wa Morelos, siku moja baada ya miili mingine tisa kupatikana katika mji jirani wa Fresnillo, mamlaka imesema.

Maafisa wa polisi wa upelelezi wakisimama karibu na miili iliyofunikwa kwa blanketi na kufunikwa kwa mkanda ulioachwa na watu wasiojulikana katika jimbo la Zacatecas, Mexico, Mei 7, 2024.
Maafisa wa polisi wa upelelezi wakisimama karibu na miili iliyofunikwa kwa blanketi na kufunikwa kwa mkanda ulioachwa na watu wasiojulikana katika jimbo la Zacatecas, Mexico, Mei 7, 2024. © Jesus Enriquez / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka inasema jimbo la Zacatecas, kaskazini mwa Mexico, linakabiliwa na ongezeko la ghasia baada ya kukamatwa kwa washukiwa wa uhalifu hivi majuzi. Katika taarifa, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Zacatecas imesema kwamba "miili tisa ilipatikana, wote wakiwa wanaume," bila kutoa maelezo zaidi.

Kuhusu miili mingine tisa iliyogunduliwa siku ya Jumanne hii, "waathiriwa watano walitambuliwa na miili ilirejeshwa kwa familia zao," kimesema chanzo hiki.

Eneo la Morelos na Fresnillo iko kwenye mhimili wa ulanguzi wa dawa za kulevya unaopiganiwa na magenge mawili ya vurugu nchini Mexico, Sinaloa na Jalisco Nueva Generacion, kulingana na mamlaka.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, makundi ya uhalifu yalifunga barabara na kuchoma magari ili kukabiliana na kukamatwa kwa washukiwa kumi na watatu wa uhalifu huko Fresnillo.

Zaidi ya watu 100,000 wametoweka tangu mwisho wa mwaka 2006

Kulingana na uchunguzi rasmi, 96% ya wakaazi wa Fresnillo wanaogopa kuwa waathiriwa wa uhalifu, na kuifanya kuwa jiji lenye kiwango cha juu zaidi cha mtazamo wa ukosefu wa usalama nchini Mexico. Na usalama ndio kiini cha kampeni ya uchaguzi wa tarehe 2 Juni.

Mgombea wa upinzani wa mrengo wa kati Xochitl Galvez alizindua kampeni yake kutoka Fresnillo, usiku wa Machi 1, kwa kuahidi kukomesha vitendo viovu vya walanguzi wa dawa za kulevya. Alilenga moja kwa moja mgombea anayepewa nafasi katika uchaguzi huo, mgombea wa mrengo wa kushoto aliye madarakani Claudia Sheinbaum, ambaye anaahidi kuendeleza sera ya rais anayemaliza muda wake Andres Manuel Lopez Obrador kwa kukabiliana na sababu za kijamii za vurugu (umaskini, kutengwa, nk).

Tangu mwisho wa mwaka 2006, mashambulizi ya kijeshi dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya yalipoanzishwa, Mexico imerekodi mauaji 450,000 na zaidi ya watu 100,000 waliotoweka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.